Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini,
Mhe Yagi Kiaratu ameandaa futari kwa wananchi wa jimbo hilo na kugawa tende
katika kata 18 za jimbo hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo Kiaratu amewashukuru wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kwa kushiriki katika futari hiyo, huku akisisitiza kutunza amani iliyopo nchini.
Kiaraatu alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi alizozitoa Mkoa wa Singida kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, alimpongeza Kiaratu, kwa kuandaa futari kwa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Dendego amesema hatua ya mbunge huyo
kuandaa futari inaonesha jinsi alivyo na moyo wa uzalendo na mshikamano miongoni mwa wananchi,
huku akisisitiza kuwa maombi yana nafasi kubwa katika kudumisha amani na
maendeleo ya taifa
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali, viongozi wa dini huku baadhi yao
wakipata nafasi ya kutoa salamu na kumshukuru mbunge huyo kwa kuandaa futari
hiyo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Shekhati wa Mkoa wa Singida, Zeana Said Salumu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Gwau akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Yagi Kiaratu akichukua chakula.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akichukua chakula.
Wakati wa kula chakula ukiendelea
Chakula kikiendelea kuchukuliwa. Huyu ndugu upande wa kulia ni kama anasema ' Niongezee kitumbua kama hiki'
Chakula kikichukuliwa.
Sheikh wa Wilaya ya Singida, Issa Simba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Eliya Digha, akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itigi na Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Yohana Msita akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu akigawa tende.
Tende zikigawiwa.
Furaha ikitawala wakati wa kukabidhiwa tende.
Ni tabasamu tu wakati wa kupokea tende kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Yagi Kiaratu
Taarifa hii imeaandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.







No comments:
Post a Comment