Naitwa Jackson, mzaliwa wa mkoa wa Mara lakini nimeishi Dar es Salaam kwa miaka kumi sasa. Nilimaliza elimu yangu ya juu nikiwa na matumaini makubwa ya kupata kazi ya maana na kuikwamua familia yangu kutoka kwenye lindi la umaskini. Lakini ndugu zangu, maisha ya jijini Dar yalinionyesha cha mtema kuni.
Kwa miaka sita, nilikuwa nikizungusha bahasha za ‘CV’ kila ofisi, kuanzia Posta hadi mitaa ya Mikocheni, lakini majibu yalikuwa ni yale yale: “Tutakupigia.”








No comments:
Post a Comment