Msomi aliyeshindwa kueleweka na wanaume, sasa hivi anadunda na mume mzungu!
--------------------------------------
Naitwa Rosemary, mwanamke ambaye nilipoteza ujana wangu wote nikisoma na kutafuta maisha, nikiamini kuwa nikishapata elimu na kazi nzuri, basi wanaume watajipanga mistari kunioa.
Lakini mambo hayakuwa hivyo hata kidogo. Baada ya kufikisha umri wa miaka 39, nikiwa na vyeo vyangu vikubwa na mshahara mnono, nilijikuta nikizungukwa na upweke uliopitiliza.
Kila mwanaume aliyekuwa anakuja kwangu, alikuwa anakaa kwa wiki mbili tu kisha anapotea bila kuaga.
Wengine walikuwa wakiniambia waziwazi kuwa nina “baridi” au ninaonekana kuwa na mambo mengi kuliko ndoa. Nilianza kuamini kuwa huenda nimerogwa kazini kwangu ili nisioewe na niishie kuwa mzee wa makaratasi tu.








No comments:
Post a Comment