Safari ya miaka sita ya maumivu
Esther Mueni, mkazi wa Kitui, anasema alikumbana na changamoto ya kupata mtoto kwa muda wa miaka sita bila mafanikio. Licha ya kuolewa na kuwa na matumaini ya kuanzisha familia, alijikuta akisubiri kwa muda mrefu bila kubeba ujauzito.
Kwa mujibu wake, hali hiyo ilimletea presha kubwa kutoka kwa jamii na hata ndugu wa karibu. Watu walikuwa wakimuuliza maswali ambayo mara nyingi yalimuumiza moyo.
Alitembelea hospitali kadhaa na kufanyiwa vipimo mbalimbali, lakini hakupewa majibu ya wazi kuhusu sababu ya hali hiyo.








No comments:
Post a Comment