.............................
Na Mwandishi Wetu.
ZAIDI ya Sh. milioni 200 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati iliyopangwa kujengwa Kigezi Chini, Buyuni, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza ofisini kwake juzi, Mwenyekiti wa Serikali wa Kigezi Chini, Musa Singano, alisema Zahanati hiyo itaanza kujengwa kwa nguvu ya wananchi.
Singano alisema baada ya serikali kuwajengea Shule ya Sekondari inayoitwa Kigezi Chini, kwa sasa wanakabiliwa na kero ya Zahanati.
Alisema kutokana na uhitaji mkubwa wa uwepo wa huduma ya afya karibu, wakazi wa Kigezi Chini wameanza kuchangia tofari 1000 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo.
Singano alisema kwa sasa wakazi wa Kigezi Chini wanategemea kupata matibabu katika Zahanati ya Kata ya Buyuni iliyopandisha hadhi ya kuwa Kituo cha Afya, ambako ni mbali.
Mwenyekiti huyo alisema pamoja na wakazi hao kuanza mchakato wa ujenzi wa Zahanati hiyo, lakini anahitaji sapoti ya serikali ili waweze kutimiza malengo yao.
"Tunaiomba serikali itusaidie baada ya wananchi kuanza kujitolea kuchangia tofari kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati yetu," alisema Singano.
Alisema pamoja na kuwapo kwa mchakato wa ujenzi wa Zahanati, lakini anaipongeza serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule ya kisasa ya Sekondari ya Kigezi Chini iliyogharimu zaidi ya Sh. 500 Milioni.
Pia alipongeza kwa kupata mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Itariani hadi Kigezi Chini ambayo itajengwa kwa fedha za UMDP.
Alisema Barabara hiyo ikikamilika itaunganisha na mitaa mingine, lakini itakuja uchumi wa wakazi wa eneo hilo.
Pia alimpongeza Diwani wa Kata ya Buyuni, Jesca Msulwa kutokana na ufuatiliaj wa maendeleo kwa hatua kwa hatua.








No comments:
Post a Comment