OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATENGA BILIONI 2.6 MRADI WA MABADILIKO TABIANCHI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, 27 March 2026

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATENGA BILIONI 2.6 MRADI WA MABADILIKO TABIANCHI

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo- Zanzibar Bw. Saleh Mohamed Juma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo- Zanzibar Bw. Saleh Mohamed Juma akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya  Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Bw. Mwalim Khamis Mwalim akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi huo kilichofanyika Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6. Kushoto ni Mratibu wa Mradi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. James Chuyi
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw James Chuyi akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mradi wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi huo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Kaninzio Manyika akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo na Uratibu wa Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Magdalena Ngotolainyo akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Lucas Sabida akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwaklilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Jackson Msagati akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Bahati Shagihilu akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma iliyokutana kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Honest Anicetus akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo-Zanzibar Bw. Saleh Mohamed Juma akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Honest Anicetus akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo wakifuatilia kikao cha kamati hiyo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Ali Vuai akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo Bw. Ali Vuai wakati wa kikao cha kamati hiyo  iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo iliyokutana Machi 27, 2026 Jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya utekelezaji wa mradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6.
------------------------------------------------------
Na Ofisi ya Makumu wa Rais

Mradi wa kuimarisha jamii pamoja na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo umepanga kutumia Shilingi Bilioni 2.6 kwa mwaka 2025/26-2026/27 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi huo.


Akifungua kikao cha kamati tendaji ya Mradi huo Machi 27, 2026 Jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amesema mradi huo unatekelezwa katika misitu ya miombo Tanzania Bara na Maeneo Kame Zanzibar.


Amesema mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais-Zanzibar, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo-Zanzibari, na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).


“Mradi huu umekusudia kuboresha na kuimarisha mazingira wezeshi ili kukuza matumizi ya teknolojia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kipaumbele hapa nchini” amesema Balozi Luvanda.


Mhe. Balozi Luvanda amebainisha kuwa mradi huo pia utaongeza mnyororo wa thamani ya mazao yasiyokuwa ya misitu, mbogamboga na malisho ya mifugo kwa ukanda wa maeneo ya miombo kwa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar.


Amesema dhamira ya Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuhakikisha inaongeza furs ana wigo wa upatikanaji wa miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini  kujenga uwezo kwa jamii zenye changamoto ya rasilimali fedha na uelewa mdogo wa mbinu za uzalishaji wa mazao.


Kwa upande wake Mratibu wa Mradi, Bw. James Chuyi amesema mradi huo unatekelezwa katika Mikoa saba iliyopo katika Halmashauri saba nchini kutoka upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.


Ameitaja Mikoa hiyo kuwa ni Tabora (Sikonge), Rukwa (Nkasi), Katavi (Mpanda), Kaskazini Unguja (Kaskazini B), Kusini Unguja (Kusini), Kaskazini Pemba (Micheweni) na Kusini Pemba (Chakechake).


Mradi wa kuimarisha jamii na mifumo ikolojia katika kuhimili mabadiliko ya tabianchi ukanda wa misitu ya miombo unatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025-2029 na unafadhiliwa wa Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) kupitia usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad