Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Singida, Petro Horombe akizungumza Machi 9, 2026 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026.
............................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 narejeo ya mwaka 2023 imefanikiwa kurejesha zaidi ya Sh. Milioni 119.
Hayo yamebainishwa Machi 9, 2026 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Petro Horombe wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/ 2026
Horombe alisema katika utekelezajı wa ma}ukumu yake TAKUKURU imefanıkiwa kusaidia kurejesha zaidi ya Sh. 119 pamoja na magari manne kutokana na kazi za uchunguzi.
“ Chambuzi za mifumo na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 25 yenye thamani ya Sh. 5,177,915,609.00 katika sekta za Elimu, Maji, Barabara, Afya, na Utawala kiasi hicho cha fedha kilirejeshwa,” alisema Horombe.
Akifafanua zaidi alisema kiasi cha Sh. S7,585,OOO.00 zilirejeshwa serikalini kutokana na chunguzi za tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa mali za umma, na magari manne baada ya uchunguzi kwa Taasisi miliki, kutokana na kuuzwa kinyume cha taratibu.
Horombe aliongeza kuwa Sh. 43,810,000.00 zililipwa kwa wazabuni kwa ajili ya kusambaza vifaa vya ujenzi lakini vifaa hivyo havikufikishwa kwenye maeneo ya miradi na baada ya ufuatiliaji, vifaa vyenye thamani hiyo viliwasilishwa kwenye miradi husika.
Aidha, alisema Mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi alijipatia isivyostahili Sh.7,531,215.00 za kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kutoa Stakabadhi ya kughushi ya EFD baada ya kupokea malipo ya vifaa alivyosambaza kwenye utekelezaji wa mradi wa maendeleo na baada ya ufuatiliaaji, mzabuni huyo aliwasilisha stakabadhi halali ikiwa na makato hayo ya kodi.
Horombe akitoa ufafanuzi zaidi alisema Sh. 2,337,000.00 zililipwa kwa mzabuni baada ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika utekelezaji wa mradi visivyo na ubora na sifa zilizotajwa kwenye mkataba na baada ya ufuatiliaji, mzabuni aliwasilisha vifaa stahiki kwa mujibu wa mkataba.
Fedha nyingine zilizorudishwa ni Sh. 2,009,884.63 za ushuru wa huduma zilichukuliwa na wazabuni waliosambaza vłfaa vya ujenzi kwenye miradi ya maendeleo isivyostahili baada ya kutokatwa kwenye malipo yao ambazo zimerejeshwa kwenye akaunti za Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri baada ya uchunguzi.
Alisema Sh. 1,563,625.25 za kodi ya zuio zilikatwa kwenye malipo ya wazabuni waliosambaza vifaa vya ujenzi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pasipo kuwasilishwa kwenye mamlaka ya Napato Tanzania (TRA) na baada ya ufuatiliaji, fedha hizo ziliwasilishwa TRA kwa mujibu wa sheria.
Wakati huo huo Horombe alisema kuwa kupitla uchambuzi wa mfumo wa vyombo vya watumia maji wameweza kurejeshwa Sh. 3,000,000.00 kwa mwananchi mmoja ambaye alilipa kiasi hicho cha fedha kimakosa kwenye akaunti ya jumuiya ya watumia maji ambapo awali uongozi wa jumuiya hiyo haukuwa tayari kurejesha fedha hizo hadi TAKUKURU ilipoingilia kati.
Mafanikio hayo ya kurejesha fedha hizo yanatokana na ushirikiano baina ya taasisi hiyo pamoja na wadau mbaalimbali.
Vijana wa Chama cha Skauti Tanzaniaa (TSA), Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habariMaafisa Usafirishaji (Bodaboda ) Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huoWanafunzi wa Shule ya Sekondaari ya Senge wakiwa kwenye mkutano huo.






No comments:
Post a Comment