𝐌𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀𝐊𝐔𝐔 𝐂𝐇𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀, 𝐙𝐀𝐍𝐙𝐈𝐁𝐀𝐑 𝐖𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐔𝐔𝐍𝐆𝐀𝐍𝐎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, 24 April 2026

𝐌𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀𝐊𝐔𝐔 𝐂𝐇𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀, 𝐙𝐀𝐍𝐙𝐈𝐁𝐀𝐑 𝐖𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐔𝐔𝐍𝐆𝐀𝐍𝐎

Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Saleh Juma Mussa akisaidiwa akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wameshiriki kikao cha kujadili Masuala ya Muungano kilichofanyika Zanzibar,  Aprili 24, 2026.
Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi akimwakilisha Katibu Katibu Mkuu Kiongozi (SJMT) kuongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wameshiriki kikao cha kujadili Masuala ya Muungano kilichofanyika Zanzibar,  Aprili 24, 2026. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi.
Viongozi mbalimbali wakishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wameshiriki kikao cha kujadili Masuala ya Muungano kilichofanyika Zanzibar, Aprili 24, 2026. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Ikulu) Bw. Mululi Mahendeka (katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa mara baada ya kikao cha Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichoketi Zanzibar 

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi (kulia) akishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichoketi Zanzibar leo, tarehe 24, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Salhina Mwita Ameir.

…………

Makatibu Wakuu wa SJMT na SMZ wakutana kujadili Masuala ya Muungano

Makatibu Wakuu wa Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wameshiriki kikao cha kujadili Masuala ya Muungano kilichofanyika Zanzibar, Aprili 24, 2026.

Kikao hicho kimeongozwa na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Saleh Juma Mussa akisaidiwa na Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim J. Yonazi akimwakilisha Katibu Katibu Mkuu Kiongozi (SJMT).

Kikao hicho ni mwanzo wa kikao cha Mawaziri wa SJMT na SMZ kinachotarajiwa kufanyika Aprili 25, 2026 kabla ya kufanyika kwa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ ambayo Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Emmanuel Nchimbi.

Katika kikao cha Makatibu Wakuu, Viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dkt. Islam Seif Salum, Wakurugenzi, Naibu Makatibu Wakuu na wataalamu kutoka Serikali zote mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad