Kulikuwa na kipindi nilihisi maisha yangu yamesimama kabisa. Kila nilichojaribu kufanya hakikuwa na matokeo yanayoeleweka.
Nilikuwa na malengo, lakini njia ya kuyafikia ilionekana kufungwa kila upande. Nilianza kazi kadhaa lakini sikudumu. Fursa zilikuja na kupotea. Hata maamuzi ya kawaida yalikuwa yananichanganya.
Nilijikuta nikizunguka kwenye mzunguko uleule bila maendeleo ya kweli. Kilichoniumiza zaidi ni kuona watu walioanza pamoja nami wakisonga mbele, wakati mimi nilionekana kubaki sehemu moja. Ilianza kunifanya nijiulize kama kuna kitu ninachokosa kabisa katika maisha yangu.
Kadri siku zilivyopita, nilianza kuona dalili ndogo ambazo mwanzoni nilikuwa nazipuuzia kama kukosa umakini, kurudia makosa yale yale, na hisia ya ndani kwamba kila kitu nilichochagua kilikuwa hakijakaa sawa.









No comments:
Post a Comment