𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐍𝐘𝐀𝐋𝐀𝐍𝐃𝐔: 𝐓𝐔𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐄 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, April 27, 2026

𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐍𝐘𝐀𝐋𝐀𝐍𝐃𝐔: 𝐓𝐔𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐄 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀

Katika kipindi ambacho dunia inaangalia mwenendo wa usalama na utulivu wa mataifa, kauli ya serikali imeendelea kuweka msisitizo mkubwa juu ya jukumu lake la msingi la kulinda maisha na mali za wananchi.

Hili limebainishwa na Mshauri wa Rais wa Diplomasia, Balozi Lazaro Nyalandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya kimataifa.

Akiweka msimamo wa serikali bayana, Balozi Nyalandu alieleza kuwa kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaakisi dhamira ya dhati ya kuhakikisha kila mwananchi anaishi salama na kulindwa bila kujali changamoto zinazojitokeza.

Ripoti ya Tume ya Jaji Chande imekuwa nyenzo muhimu katika kuweka wazi ukweli ambao kwa muda ulikuwa ukizua maswali miongoni mwa wananchi,
“Kupitia uchunguzi wa kina, tume hiyo imeweka hadharani mambo muhimu, ikiwemo hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na hali hiyo, hii ni ishara ya uwajibikaji na uwazi unaopaswa kupongezwa”,

Alieleza kuwa kwa muktadha huu, ni muhimu kwa jamii kutambua tofauti kati ya haki ya kuandamana kwa amani na vitendo vya vurugu vinavyohatarisha usalama wa taifa.
Amesema wananchi wanapaswa kuwa macho, kushirikiana na vyombo vya dola, na kuepuka kushawishiwa kujiingiza katika matendo yanayoweza kuleta madhara makubwa.

Ulinzi wa taifa si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja wetu hivyo tukishirikiana tunaweza kujenga jamii yenye amani, mshikamano, na maendeleo endelevu.

Ni wakati wa kusimama pamoja, kuilinda nchi yetu, na kuhakikisha kuwa mustakabali wa vizazi vijavyo unabaki salama na thabiti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad