𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔 𝗠𝗙𝗔𝗡𝗢 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗔𝗠𝗕𝗔𝗡𝗢 𝗗𝗛𝗜𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗛𝗔𝗥𝗔𝗠𝗨 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 22 April 2026

𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔 𝗠𝗙𝗔𝗡𝗢 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗔𝗠𝗕𝗔𝗡𝗢 𝗗𝗛𝗜𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗕𝗜𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗛𝗔𝗥𝗔𝗠𝗨

---------------------------
Na Mwandishi wetu -  Singida


Timu kutoka Uganda ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Malikale Bi. Doreen S. Katusiime yafanya ziara ya mafunzo Itigi.

Timu hiyo ipo nchini Tanzania na jumanne  Aprili 21,2026 imetembelea vikundi na miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya mradi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara ( IWT Project).

Miongoni mwa vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na Jumuiya ya wafuga nyuki Muhesi na kikundi cha Nyukimali Doroto Itigi mkoani Singida.

Huu ni mpango maalumu wa ziara za mafunzo baina ya nchi zinazotekeleza Miradi yenye malengo yanayoshabihiana ili kubailishana uzoefu na kujifunza namna nchi nyingine inavyotekeleza Mradi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad