ELIMU BIASHARA YA KABONI KUIMARISHWA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, April 17, 2026

ELIMU BIASHARA YA KABONI KUIMARISHWA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akijibu maswali bungeni jijini Dodoma Aprili 17, 2026.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Ridhiwani Kikwete bungeni jijini Dodoma Aprili 17, 2026. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Mathew.
------------------------------

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu dhana, faida na fursa zilizopo katika biashara hiyo kupitia vyombo vya habari na kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi za mikoa, halmashauri na vijiji ili waweze kuwa mabalozi wa elimu kwa jamii zao kuhusu utekelezaji wa miradi ya kaboni na manufaa yake.


“Tangu kupitishwa kwa Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni tumetoa elimu kwa viongozi mbalimbali pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na sekta binafsi katika kutoa elimu na kujenga uwezo kwa jamii kuhusu namna ya kuanzisha na kunufaika na miradi ya kaboni,” alisema Mhe. Kwagilwa.


Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwagilwa alisema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinashirikiana katika kutekeleza miradi ya mazingira na kunufaisha wananchi wa pande zote mbili za Muungano.


Alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Amani Mhe. Abdul Yussuf Maalim aliyetaka kufahamu Zanzibar inanufaika vipi na biashara ya kaboni.


Akiendelea kujibu swali hilo, Mhe. Kwagilwa alisema pamoja na kushirikiana katika biashara ya kaboni pia Serikali zote mbili zinashirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


Ikumbukwe kuwa biashara ya kaboni ni mfumo wa kifedha unaoruhusu nchi, taasisi au miradi kupunguza uzalishaji wa gesi joto na kupata faida kwa kuuza au kubadilishana hati za kaboni ambazo hutolewa unapofanikiwa kupunguza au kufyonza hewa ya kaboni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad