Katika kuelekea Matembezi ya Mshikamano kwa Afya ya Ubongo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 12 Aprili 2026, juhudi za kuelimisha na kuhamasisha jamii zimeendelea kuimarika, huku Kituo cha Bodaboda Muhimbili kikiwa miongoni mwa maeneo yaliyofikiwa na ujumbe muhimu wa usalama barabarani.
Katika shughuli hiyo, madereva wa bodaboda wawakilishi kutoka Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kuvaa helmet kwa dereva na abiria. Elimu hiyo imelenga kulinda ubongo na kuzuia majeraha ya kichwa yanayotokana na ajali za pikipiki.
Akizungumza na madereva hao, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Rahma Hingora, amesisitiza kuwa matumizi ya helmet si hiari bali ni hatua muhimu ya kuokoa maisha.
“Ubongo hauna spea. Ni muhimu kwa dereva na abiria kuhakikisha wanavaa helmet kila safari—iwe ndefu au fupi—ili kujilinda na majeraha ya kichwa yanayoweza kubadilisha maisha ghafla,” alisema Dkt. Hingora.
Aidha, aliwahimiza bodaboda hao kushiriki kikamilifu katika matembezi hayo yatakayoanzia Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akieleza kuwa tukio hilo ni fursa ya kujifunza zaidi, kuhamasisha jamii, na kuchukua hatua madhubuti za kulinda maisha.
Dkt. Hingora pia aligusia umuhimu wa madereva wa bodaboda kujiunga na bima ya afya, akieleza kuwa ni kinga muhimu dhidi ya gharama kubwa za matibabu pindi ajali zinapotokea. Aliongeza kuwa madhara ya ajali hayaishii kwa mhusika pekee, bali huathiri familia na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI), Dkt. Juma Magogo, alieleza kuwa majeraha ya kichwa yana athari kubwa kiafya na kiuchumi, na mara nyingi husababisha ulemavu wa kudumu.
“Gharama za matibabu ya majeraha ya kichwa ni kubwa, na wakati mwingine madhara yake hayawezi kurekebishwa. Ni muhimu kuchukua hatua mapema kinga ni bora kuliko tiba,” alisisitiza Dkt. Magogo.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Kagomba, aliipongeza Serikali kwa juhudi za kuelimisha bodaboda na kuahidi kuendelea kusambaza ujumbe huo kwa wanachama wake.
“Tunaishukuru Serikali na wadau wote kwa elimu hii. Tutaendelea kuwahamasisha wanachama wetu kuvaa helmet na kuzingatia usalama barabarani ili kuokoa maisha,” alisema Kagomba.
Matembezi hayo yanatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha matumizi ya helmet na kuchochea mabadiliko ya tabia kwa jamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza majeraha ya kichwa yanayotokana na ajali za pikipiki nchini.

.png)

No comments:
Post a Comment