KATIBU MKUU CCM AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA JUMUIYA YA MADOLA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, April 15, 2026

KATIBU MKUU CCM AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA JUMUIYA YA MADOLA

.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 15 Aprili 2026 amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera, katika Ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mhe. Chakwera yupo nchini Tanzania kwa ziara maalum katika nafasi yake kama Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey.

Kikao hicho ni sehemu ya mashauriano yake na wadau mbalimbali wa kitaifa kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, pamoja na juhudi zinazoendelea za kuimarisha amani, demokrasia na mshikamano wa kitaifa nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad