Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa (Kushoto), na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Bi. Pili Mbanga, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mhe. Balozi Omar kutembelea Ofisi za Chama hicho, ngazi ya Mkoa kujitambulisha baada kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Waziri wa Fedha.
---------------------------------
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa, alipotembelea Ofisi za Chama hicho, ngazi ya Mkoa, kujitambulisha.
“Nimekuja kwenye Ofisi za Chama kujitambulisha baada kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Waziri wa Fedha, ni mkazi sasa wa Dodoma, mwanachama hai wa CCM, nikaona ni vema nije kujitambulisha” Alisema Mhe. Balozi Omar
Alisema kuwa CCM ndiyo inayoongoza Serikali baada ya kuchaguliwa na wananchi na Ilani ya Chama ndiyo inayotekelezwa, hivyo ni utamaduni wangu kwamba kila nitakapopata fursa ya kutembelea mikoani, pamoja na kuwatembelea Wakuu wa mikoa, nitapita pia kujitambulisha kwenye Ofisi za Chama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa, aliyeambatana na Katibu wa CCM wa mkoa huo Bi. Pili Mbanga, alimpongeza na kumsifu Mhe. Balozi Omar kwa moyo wake wa kipekee wa kutambua umuhimu wa Chama katika kutekeleza majukumu yake.
“Nitumie fursa hii kukupongeza, umeanza vizuri sana, uko tofauti sana na wengine, we are proud of you! umeonesha mfano usio wa kawaida na wewe ni mtu wa kipekee sana, tutakupa ushirikiano” Alisema Alhaji Kimbisa.
Alhaji Kimbisa alisema kuwa Chama cha Mapinduzi mkoani Dodoma kiko imara na kinaendelea kuwatumikia wananchi kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa huduma muhimu za jamii zinatolewa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Chama cha Mapinduzi kinaamiwa na kiko madarakani mpaka leo ni kwa sababu kinawasikiliza wananchi, wakisema wanataka maji, shule, barabara, hospitali, Serikali ya CCM inapeleka” aliongeza Alhaji Kimbisa.
Mbali na kuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, ni Miongoni mwa Wajumbe watano wanaoliwakilisha Bunge katika Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

No comments:
Post a Comment