MWENYEKITI KAMATI YA USTAWI WA JAMII BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR AIPONGEZA MSD - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, April 16, 2026

MWENYEKITI KAMATI YA USTAWI WA JAMII BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR AIPONGEZA MSD

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hussein Ibrahim Makungu, akiwa kaatika picha ya pamoja na wajumbe wake.
.............................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hussein Ibrahim Makungu ameippngeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa maboresho makubwa iliyofanya kuwezesha kuimarika kwa mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, hasa kuwezesha vifaa na mashine za kisasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Mwenyekiti huyo na wajumbe wake ambao wamefanya ziara ya kubadilishana uzoefu na Bohari ya Dawa (MSD) wameeleza kuwa, MSD kusambaza bidhaa za afya kwa vituo 8,900 nchi nzima hadi mlangoni kwa mteja mara sita kwa mwaka ni hatua kubwa, na ya kupongezwa.

Ameongeza kuwa, vifaa vya kisasa na vinavyoendana na teknolojia ya kisasa vinavyonunuliwa na serikali kupitia MSD na kuwezesha matibabu ya kitaalam kufanyika nchini ni jambo la kujivunia, kwani wananchi sasa wanapata huduma nyingi za kibingwa ndani ya nchi.

Kwa upande mwingine, wamepongeza juhudi za ujenzi wa maghala mapya na ya kisasa Mkoani Dodoma na Mtwara ambayo yameongeza ukubwa wa mita za mraba 12,000 na kuongeza uwezo wa uhifadhi na huduma kwa wananchi, huku ujenzi mwingine ukiendelea Wilayani Chato.

“Tuna la kujifunza hapa kwani huko Zanzibar Bohari Kuu ya Dawa ina changamoto ya eneo la uhifadhi wa bidhaa za afya, na zipo nyingi” alisema Mhe. Makungu”.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Elisamehe Macha ameeleza kuwa maboresho ya huduma za MSD yanaendana na malengo ya serikali ya kusogeza huduma kwa wananchi, ndio maana MSD imenunua na kusambaza bidhaa za huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo, kinywa na meno, vifaa vya upasuaji, mashine za uchunguzi, pamoja na mama na mtoto.

Ameongeza kuwa, hali ya upatikani wa bidhaa za afya pia imeimarika, kwani kwa sasa MSD inakidhi mahitaji ya wateja kwa wastani wa asilimia  83.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikifanyika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad