..................................
Na Mwandishi Wetu.
WAMILIKI wa shamba lenye heka 90 Iililoko Mtaa Somelo, Kata ya Zingiziwa , Ilala, Dar es Salaam, wamelalamikia kuwapo kwa mtu aliyetajwa Obadia Mkwabi akidaiwa kuvamia maeneo yao na kuyakatakata vipande kwa lengo ya kuuza viwanja.
Hata hivyo wanakusudia kumfikisha mvamizi huyo katika Mahakama Kuu ya Ardhi Tanzania ili aweze kujibu kesi kuhusiana na uhalali wa kulipata shamba hilo.
Wakizungumza Mei 2, mwaka huu, mmoja wa wamiliki wa shamba hilo, Alfonce Malya, alisema mtu huyo anashirikiana na baadhi ya viongozi waliopewa mamlaka ya kuongoza nchi ili kuwadhulumu haki yao.
Malya alisema shamba hilo, alinunua mwaka 1990, akiwa hajastaafu katika utumishi wa umma.
Alisema baada ya kununua shamba hilo na jirani yake, Florian Bubelwa, wanashangaa kuona Mei mosi, mwaka huu, mvamizi huyo kwenda kupima shamba lao kwa lengo kujua ukubwa wake kwa lengo la kukata viwanja.
Mmiliki wa shamba hilo, alisema baada ya mwaka 2001 kwenda India kutibiwa alikaa muda mrefu bila kufika shambani kwake na mvamizi huyo alitumia fursa hiyo kutaka kujimilikisha shamba hilo.
Malya alisema mvamizi huyo anashirikiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa kutaka kupora mali yao.
Naye, Florian Bubelwa, ambaye ni mmoja wa mmiliki wa shamba hilo, alisema alinunua ardhi hiyo 1988 kabla ya kustaafu katika utumishi wa umma.
Bubelwa alisema anavyo vieleezo vyote vinavyoonesha uhalali wa kumiliki shamba hilo.
Alisema kutokana na kuwapo kwa tukio hilo anakusudia kwenda mahakamani ili haki iweze kutendeka.
Bubelwa alisema akiwa mmiliki halali wa shamba hilo, ataendelea kulihudumia na kama kuna mtu anadai la kwake atathibitisha mahakamani.
Mmiliki wa shamba hilo kwa sasa alisema tayari amewasiiana na mwanaheria wake kwa lengo la kulipeleka suala hilo mahakamani.
Kwa upande wake Mkwabi alidai kuwa shamba hilo ni lake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Somelo, Hasan Rashid, alisema amepata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu madai ya shamba hilo, ingawa mlalamikiwa hajawahi kufika ofisini kwake.









No comments:
Post a Comment