𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐙𝐀 𝐋𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎, 𝐔𝐖𝐄𝐊𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, May 7, 2026

𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐙𝐀 𝐋𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎, 𝐔𝐖𝐄𝐊𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi  Mei 7, 2026, ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kimataifa unaowakutanisha Wadau wa Utalii Duniani chini ya Baraza la Usafiri na Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika ndani ya meli ya Crystal Serenity inayosafiri kutoka bandari ya Sokhna kuelekea Alexandria nchini Misri.


Kupitia Mkutano huo Dkt. Abbasi amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo Bi. Gloria Guevara, Waziri wa Zamani wa Utalii wa Mexico akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Bw. Najib Balala, Waziri wa Zamani wa Utalii wa Kenya ambapo wamejadili masuala mbalimbali na namna Baraza hilo linavyoweza kusaidia kuendeleza Sekta ya Utalii nchini katika maeneo ya mafunzo, teknolojia na uwekezaji.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Richard M. Makanzo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad