𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐊𝐎𝐌𝐁𝐎 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐃𝐇𝐀𝐑𝐔𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐒𝐀𝐃𝐂 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, May 10, 2026

𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐊𝐎𝐌𝐁𝐎 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐃𝐇𝐀𝐑𝐔𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐌𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐒𝐀𝐃𝐂

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi, na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-MCO), uliofanyika  tarehe 10 Mei, 2026, Jijini Nairobi, Kenya.

Mkutano huo uliolenga kuimarisha misingi ya amani, umeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. George Chaponda, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Malawi.

Katika mazungumzo hayo, Mawaziri wamejadili changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili kanda hiyo ikiwemo Vurugu zinazoendelea nchini Afrika Kusini dhidi ya raia wa nchi nyingine za Afrika.

Kwa Upande wake Mwenyekiti Dkt. Chaponda amewahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa mapendekezo yote yaliyofikiwa yatafanyiwa kazi kwa haraka na kwa ufanisi. Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya SADC kuhakikisha kuwa Kanda ya Kusini mwa Afrika inasalia kuwa kisiwa cha amani, utulivu, na ushirikiano wa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad