Kikao kazi hicho kilichowashirikisha pia wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI); Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kilicholenga kujadili utekelezaji wa Progamu ya ‘Otesha Afrika’ inayohusu uhamasishaji na upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali nchini.
Akifungua kikao hicho, Dkt. Manyika alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha jukumu la kulinda na kuhifadhi mazingira linakuwa endelevu.
Alieleza kuwa Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ambayo inaweza kugeuka fursa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kampeni za upandaji wa miti.
“Sote tunatambua kuwa kila tarehe 17 ya mwezi Juni tunaadhimisha Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kuongezewa nguvu na ushiriki wa wadau katika kampeni za upandaji wa miti,” alisema.
Kwa upande wake Bw. Rumisho Shikonyi kutoka Taasisi ya Kazzi Africa Holdings (T) Ltd. aliomba pawepo na nguvu ya pamoja kati ya Serikali na wadau kuhakikisha utamaduni wa upandaji wa miti na kuitunza unakuwa endelevu.
Walisema ili kufanikisha malengo hayo walihimiza uwekezaji wa elimu ya upandaji wa miti hususan kwa kundi la watoto na vijana ambao ni idadi kubwa.
Aidha, washiriki wa kikao hicho wamejadiliana kuhusu usimamizi na ufuatiliaji wa miti inayopandwa na takwimu zake pamoja na ushirikishwa wa wadau katika shughuli za upandaji wa miti.










No comments:
Post a Comment