𝐖𝐈𝐙𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐋𝐈𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈 𝐌𝐆𝐔𝐔 𝐒𝐀𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐄𝐓𝐈 𝐘𝐀𝐊𝐄 𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐊𝐀 𝐖𝐀 𝐅𝐄𝐃𝐇𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔/𝟐𝟎𝟐𝟕 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, May 3, 2026

𝐖𝐈𝐙𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐋𝐈𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈 𝐌𝐆𝐔𝐔 𝐒𝐀𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐄𝐓𝐈 𝐘𝐀𝐊𝐄 𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐊𝐀 𝐖𝐀 𝐅𝐄𝐃𝐇𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔/𝟐𝟎𝟐𝟕

Waziri wa Maliasili na Utalii, Ashatu Kijaji (Mb), ameongoza kikao kazi cha maandalizi ya bajeti ya Wizara hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la bajeti la mwaka wa fedha 2026/2027 linaloendelea Jijini Dodoma.


Dkt. Kijaji anatarajiwa kuwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya mapato na matumizi ya wizara pamoja na Taasisi zake jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Wizara kuhakikisha bajeti yake inaakisi mahitaji halisi ya wananchi na kuendana na matarajio yao.

“Ni muhimu sana kuwa na hisia za wananchi wetu, hasa kujua wanahitaji nini na sisi tujipange vipi ili kufikia malengo yao. Hii ina maana kuwa na hotuba ya bajeti yenye jicho la wananchi,” amesema Dkt. Kijaji.

Aidha, amezitaka Taasisi, Idara na Vitengo zilizo chini ya wizara hiyo kuwasilisha mambo matatu makubwa waliyotekeleza kwa mafanikio katika mwaka wa fedha 2025/26, pamoja na kuainisha vipaumbele vitatu kwa mwaka 2026/27 vitakavyowanufaisha wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, amesema kikao hicho ni sehemu ya maandalizi muhimu ya bajeti, yakilenga kuweka mikakati madhubuti ya kukuza sekta ya uhifadhi, maliasili na utalii ili kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

Ameongeza kuwa bajeti hiyo pia imezingatia mipango ya kuongeza idadi ya watalii katika matukio na mikutano ya Kimataifa yatakayofanyika hapa nchini ikiwemo michuano ya AFCON 2027 pamoja na kuimarisha juhudi za uhifadhi, ili kuchochea maendeleo ya sekta husika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad