Biashara yangu ilikuwa kila kitu kwangu. Niliitegemea kulipa kodi, kulea familia, na kujisitiri kila siku. Kwa muda mrefu mambo yalikuwa yanaenda vizuri, si kwa utajiri mkubwa, lakini nilikuwa napata kile cha kuniwezesha kuendelea. Lakini ghafla hali ilibadilika. Wiki moja ilipita bila mauzo ya kueleweka.
Nilidhani ni kawaida tu, labda watu hawakuwa na pesa kipindi hicho. Lakini wiki ya pili ilipofika, hali ikawa mbaya zaidi. Nilikuwa nafungua duka asubuhi na kukaa hadi jioni bila mteja hata mmoja wa maana. Kilichoniumiza zaidi ni kuona maduka yaliyokuwa yamenizunguka yakipata wateja kawaida huku langu likiwa kimya kana kwamba halionekani.









No comments:
Post a Comment