𝐇𝐎𝐓𝐄𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐃𝐀𝐑, 𝐌𝐎𝐑𝐎𝐆𝐎𝐑𝐎 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐊𝐔𝐏𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐊𝐔𝐄𝐋𝐄𝐊𝐄𝐀 𝐀𝐅𝐂𝐎𝐍-𝟐𝟎𝟐𝟕 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 2, 2026

𝐇𝐎𝐓𝐄𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐃𝐀𝐑, 𝐌𝐎𝐑𝐎𝐆𝐎𝐑𝐎 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐊𝐔𝐏𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐊𝐔𝐄𝐋𝐄𝐊𝐄𝐀 𝐀𝐅𝐂𝐎𝐍-𝟐𝟎𝟐𝟕

IDARA ya Utalii kwa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatarajia kuanza mchakato wa kupanga hadhi (Grading and regrading) kwa watoa huduma wa hoteli na chakula nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Mei Mosi, 2026, na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Dkt. Thereza Mugobi, mchakato huo ambao ni wa kawaida ni hatua muhimu ya kujiandaa na ongezeko kubwa la wageni linalotarajiwa kuingia na kuhudumiwa nchini wakati wa michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2027)

Pia amesema unalenga kuinua ubora wa huduma ili kuiwezesha Tanzania kujitangaza kimataifa kama kitovu cha utalii na ukarimu barani Afrika huku akidokeza kuwa zoezi hilo litaanza mwanzoni mwa mwezi Mei hadi Juni 2026 katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro.

Zoezi hilo litahusisha ukaguzi wa kina wa miundombinu, usafi, ubora wa chakula, pamoja na huduma kwa wateja ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.

Amewataka wamiliki na watoa huduma wa hoteli kutumia fursa hiyo kujipima kiwango cha ubora wa huduma huduma wanazotoa ili kuvutia na kuwahifadhi wageni kabla, wakati na baada ya AFCON-2027.

Kupitia zoezi hilo, hilo hadhi ya nyota kwa hoteli itatolewa huku likizingatia ubora wa hadhi ya nyota 5 ambapo zilizokidhi zitapandishwa hadhi na zile zisizokidhi zitashushwa hadi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad