Mhaidrolojia wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Ally Diwani akiwaelezea waandishi wa habari namna wanavyopima kiwango cha maji kwenye bonde hilo.
l
Na Selemani Msuya, Iringa
BODI ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB) imesema ilikuhakikisha uwekezaji mkubwa wa miradi mbalimbali yauzalishaji inakuwa endelevu wanatarajia kuajiri walinzi50 ambao watalinda vyanzo mbalimbali vinavyotiririshamaji eneo hilo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa RBWB,Florence Mahay wakati akizungumza na waandishi wahabari kutoka katika vyombo vya habari mbalimbaliambao wapo kwenye ziara ya kutembelea bodi hiyo.
Mahay alisema bonde hilo linapokea maji kutoka mitomikubwa minne ambayo ni Ruaha Mkuu, Kilombero,Luwegu na Rufiji.Mkurugenzi huyo amesema kutokana na faida ambazozimeonekana na zinaendelea kuonekana wamejipangakuongeza ulinzi kwenye bonde hilo ambapo katikamwaka wa bajeti wa 2023/2024 wanatarajia kuajiriwalinzi 50 ambao watalinda vyanzo vilivyopo.
Amesema wamejipanga kulinda vyanzo vya majivinavyoingiza maji katika bonde hilo, ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi zilizopo zinakuwa endelevu, kwakuwa zinachangia ukuaji wa uchumi.
Mahay amesema bodi hiyo ina kazi moja kuu yausimamizi wa rasilimali za maji, kwa kuhakikishawanatambua kiasi cha rasalimali maji kwenye bonde hilo,kugawa maji, kutunza vyanzo vya maji na kuzuiauchafuzi.
Mkurugenzi huyo amesema wamelazimika kuwapitishawaandishi wa habari katika maeneo ya Bonde la Rufiji, ilikuhakikisha umma unapata taarifa sahihi katika eneo hilo.
“Serikali imewekeza katika Bonde la Rufiji kwa kujuengamiradi ya kuzalisha umeme, kama Bwawa la Mtera,Kidatu na Kihansi na kwa sasa Mradi wa UzalishajiUmeme wa Mwalimu Nyerere (JNHPP). Miradi yote hiyoina mchango katika uchumi wa nchi kama unavyoonaasilimia 80 ya umeme wa maji unatokea hapo.Lakini pia ukubwa wa bonde hili unachangia asilimia 50 ya miradi kilimo cha umwagiliaji, kama chai na sukari,hivyo tunakuwa na usalama wa chakula na tuna mbuga zawanyama takribani sita,” amesema.
Mahay amesema kwa sasa Bonde la Rufiji lina maji yakutosha ambapo kuna mita za ujazo bilioni 40, mita za ujazo bilioni 31 juu ya ardhi na bilioni 9 ni chini ya ardhi,huku maji yanatumika kwa kutolewa vibali ni mita zaujazo bilioni 2.4.
Amesema kwa sasa bodi hiyo imesitisha utoaji wa vibalivya maji ikiwa ni maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan,ili kuhakikisha maji yanajaa kwenye Bwawa la Nyerereambalo linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115.
Mahay amesema bodi hiyo haitasita kubomoamiundombinu ya wale ambao watabainika kutumia majibila kupewa vibali, hivyo wataka wananchi hasa jumuiyaza watumiaji maji kutoa taarifa pale wanapobaina.“Naomba nisisitize kuwa bodi hii haitamvumilia mtu yoyote anashiriki kutumia maji bila kibali, jumuiya zawatumia maji tunaziomba ziendelee kutoa ushirikiano, ilikuhakikisha uwekezaji unaofanywa na serikali unakuwaendelevu,” amesema.
Kwa upande wake Mhaidrolojia wa RBWD Ally Diwani,amesema kitengo chao kina vituo 137 ambapo vituo 59vinapima maji juu ya ardhi, 29 chini ya ardhi na 49 vyahali ya hewa.Amesema katika eneo hilo wana changamoto ya uharibifuwa vituo, wizi na uvunjaji wa vifaa vinasaidia kuchukua takwimu kwa ajili ya tathminj ya rasilimali maji kwenyebonde.
Naye Msimamizi wa Kitengo cha Ugawaji RasilimaliMaji wa Bodi, Mhandisi Gallus Ndunguru amesema hadisasa wametoa vibali 2005 kwa watumiaji maji mbalimbaliwalioko katika eneo la bonde.“
Pia tumetoa vibali 10 vya kutiririsha maji taka kwataasisi mbalimbali ambao wanatoa huduma zao kwakutumia maji. Ila kwa sasa tumesitisha kutoa vibali vyawawekezaji wakubwa hasa katika maeneo ambayoyameathirika,” amesema.
Ofisa Maendeleo ya Jamii RBWB, Upendo Lugallaamesema katika kuhakikisha bonde hilo linakuwaendelevu wanataerajia kupata miti 200,000 rafiki na maji.Amesema pia kupitia idara yao wamefanikiwa kuundajumuiya 42 za watumiaji maji ambao wanashiriki kulindavyanzo vya maji katika bonde hilo.
Mhandisi wa Maji, Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Gallus Ndunguru, akiwaelezea waandishi wa habari namna wanavyotoa vibali vya maji kwenye bonde hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Florence Mahay akifafua jambo mbele ya waandishi wa habari waliotembeleofisi za bonde hilo mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Florence Mahay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati yao ya kulinda bonde hilo, ili liwe endelevu.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Upendo Lugalla akielezea namna idara yao inavyotoa elimu ya utunzaji rasilimali maji
0 Comments