Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Severe Tukai, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Aprili 6, 2023 katika semina iliyoandaliwa na MSD ambayo inafanyika mkoani Dodoma.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
BOHARI ya Dawa (MSD) inatarajia kuanza kujiendesha kibiashara baada ya
kuanzisha kampuni tangu ambayo itasimamia uendeshaji wa viwanda vya taasisi
hiyo kwa ufanisi
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja, Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji wa MSD, Hassan Ibrahim wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Aprili 6, 2023 katika semina iliyoandaliwa na MSD ambayo inafanyika mkoani Dodoma.
Ibrahim alisema kuanzishwa kwa kampuni hiyo kutaifanya MSD kuingia kwenye
ushindani wa kibiashara na kuanza kujitangaza kupitia kampuni hiyo tanzu.
Alisema kupitia kampuni hiyo ambayo itakuwa na chapa yake itajitangaza na
kuitangaza MSD pamoja na kuikinga kutokana na madhara yoyote ya kibiashara
ambayo yanaweza kutokea dhidi yake.
Akizungumzia viwanda viwili ambavyo vinaendeshwa na MSD kiwanda cha mipira ya mikono vilivyopo Idofi
Makambako mkoani Njombe na cha barakoa kilichopo Keko alisema viwanda hivyo
vinamilikiwa na Serikali kupitia Bodi ya Dawa (MSD) na kuwa na eneo la barako
Serikali inaokoa Sh. Bilioni 2.9 kwa mwaka na kwa mipira ya mikono ni Sh.
Bilioni 24 fedha ambazo zingetumika kuagiza dawa na mipira hiyo nje ya nchi.
Alisema utengenezaji wa barakoa bei yake imeshuka kutoka Sh.1600 hadi
kufikia Sh. 500 baada ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho.
Ibrahim alisema uwekezaji wa Sh. Bilioni 1.4 kiwanda hicho umeleta mafanikio makubwa kwa
wananchi na moja ya faida yake ni kutoa ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Severe Tukai alisema kuanza kuendesha kibiashara inahitajika ushirikiano mkubwa katika kazi hiyo hasa kutokana na ile dhana iliyojengeka kuwa taasisi za serikali haziwezi kuanzisha jambo na kufanikiwa kujiendesha kibiashra kama ilivyo kwa makampuni ya watu binafsi.
Kiwanda hicho cha mipira ya mikono kinategemea kuzalisha mipira ya mikono milioni 86.4 kwa mwaka na mahitaji ya nchi ni milioni 104 kwa mwaka na kuwa kitazalisha asilimia 83.4 ya mahitaji hayo.
Mkurugenzi wa MSD, Severe Tukai akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya wahariri. Kulia ni Mwenyeiti wa semina hiyo, Mgaya Kingoba.
Kaimu Meneja, Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji wa MSD, Hassan Ibrahim akizungumza na wahaririAfisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka akizungumza kwenye semina hiyo.
0 Comments