MAHAKIMU 378 WAMLILIA RAIS SAMIA KUPANDISHWA MADARAJA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, May 26, 2023

MAHAKIMU 378 WAMLILIA RAIS SAMIA KUPANDISHWA MADARAJA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan
Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma. 

Na Claudia Kayombo, Singida

MAHAKIMU 378 wa mahakama za mwanzo nchini wamemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwapandisha madaraja.

Miongoni mwa mahakimu hao wapo waliopo kazini kwa zaidi ya miaka 15 ambao wamekuwa wakisubiri huruma ya serikali ya kupandishwa madaraja bila mafanikio.

Miongoni mwa mahakimu hao wamebainisha hayo hivi karibuni huku wakionesha barua iliyoandikwa Oktoba 31, 2018 na kusainiwa na aliyekuwa kaimu mtendaji mkuu wa mahakama Nyimbi iliyokuwa inakwenda Utumishi na Utawala bora ikiwaombea kupandishwa madaraja lakini hadi leo hakuna aliyepandishwa.

Barua hiyo imeainisha kuwa mahakimu wa daraja la kwanza 198 waliopata cheo cha sasa kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 wanaomba kuwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo wakuu nyongeza A huku mahakimu wa mahakama za mwanzo daraja la kwanza 88 waliopata cheo cha sasa mwaka 2010 wanaomba kuwa mahakama wa mahakama za mwanzo wakuu daraja la Pili nyongeza B.

Pia mahakimu waandamizi 54 waliopata cheo cha sasa kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 wanaomba kuwa mahakimu wa mwanzo wakuu nyongeza C.

Aidha, mahakimu wa mahakama za mwanzo wakuu 28 waliopata cheo cha sasa mwaka 2007 hadi 2010 wanaomba  kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo wakuu I nyongeza D.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad