Na Said
Hauni, Lindi.
WACHUUZI wa Samaki wabichi soko la Manispsa ya
Lindi,wamenusulika Kifo kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua paa
la jengo na kudondoshea jengo lingine na kuwaacha watu waliokuwa wanajikinga na
mvua kuendelea Kilwa na maji.
Kwa mujibu wa wachuuzi waliokuwepo sokoni
hapo,wameeleza mvua iliyoambatana na upepo ilinyesha kwa masaa mawili kuanzia
saa nane hadi tisa mchana.
Wakielezea tukio hilo,baadhi ya wachuuzi hao Juma
Isumaili,Ashura Ally,Mariamu na Mohamedi Bofu wanasema mvua hiyo imetokea
mashariki mwa Bahari ya Hindi kuelekea magharibi.
"Tukiwa tunanadisha samaki upande wa
mashariki wingu lilitanda na mvua kunyesha"Wakaeleza wachuuzi hao.
Issa Bakari Bofu akasema wakiwa ndani ya jengo
hilo,upepo mkali ulijitokeza na kuezua paa la Banda walimokuwa wamejihifadhi na
watu wengine wakiwemo wachuuzi na wanunuzi upepo ukubomoa bati na kupeleka
jengo lingine na kuachwa wakiendelea kulowa maji ya mvua.
Alisema licha ya uharibifu huo,hakuna mtu
aliyejeruhiwa kwa kukatwa na mabati ya paa hiyo.
Mwenyekiti wa Soko hilo Naibu Abdallah
Masera anakili kuwepo kwa tukio
hilo na kueleza anamshukuru mwenyezi mungu hakuna aliyekumbwa na kazia hiyo
licha ya uwepo ya idadi kubwa ya watu waliokuwa wamejihifadhi ndani ya banda
hilo.
Afisa uvuvi wa Soko hilo, Abdull Twahili amesema
upepo huo umesababisha hasara ambayo bado haijaweza kufahamika mara moja hadi
hapo wathamini watakapokamilisha kazi yao.
"Kweli hasara ipo tena kubwa tu,kwani
yanahitajika bati,boriti na misumali kwa ajili ya utekelezaj wa
paa"Alisema Twahili.
Mkurugenzi wa Manispaa Lindi,Juma Mnwele hakuweza kupatikana kuzungumzia mikakati ya matengenezo ya jengo hilo,baada ya kuelezwa yupo safarini.








No comments:
Post a Comment