Mkuu wa Mkoa Singida Peter Serukamaba (katikati) akikangua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida ya Solya inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambapo hakuridhishwa na kasi ya ujenzi huo kutokana na usimamizi hafifu wa viongozi wa halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi, Jimson Mhagama (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Jumanne Mlagaza.
........................................
Na Dotto Mwaibale- SINGIDA
MKUU wa Mkoa Singida Peter Serukamaba amesema kwamba hata endelea kuhimiza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida ya Solya inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kufuatia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Jimson Mhagama kulalamikiwa kushindwa kutekeleza maagizo yake kuhusu ujenzi huo na kusababisha usuesue,
"" Nimefika hapa sina mpango wa kuzungumza tena nimeona nipeleke ujumbe kwa Waziri wa TAMISEMI na neno langu ni moja tu kama hamjamaliza mtajuana naye binafsi nimeshindwa kuhusu wewe na sina mamlaka na wewe na kila ninalolifanya nyie hamlitaki mnafanya mnayotaka nyinyi nashukuru,''' alisema Serukamba.
Ukaguzi wa ujenzi huo ukiendelea.
RC Serukamba (kushoto) akiongoza ukaguzi wa ujenzi huo.
..............................................
ANGALIA VIDEO CHINI







No comments:
Post a Comment