Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, akizungumza wakati akifungua kikao cha 22 cha Baraza la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD), Mjini Morogoro Disemba 15, 2023.
...............................................................
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu
ameilekeza Bohari ya Dawa (MSD) kuwajali wateja na kuwashirikisha katika suala
zima la kuwapa huduma za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.
Dkt. Jingu ambaye alifungua rasmi kikao cha
ishirini na mbili (22) cha baraza la
Wafanyakazi la MSD mjini Morogoro amesisitiza kuwa, kujali wateja ni msingi
wa kuwahudumia wateja kulingana na
mahitaji yao.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amesisitiza MSD kujiendesha
kibiashara na kuwa wabunifu ili kuweza kuleta ufanisi na tija.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Ndugu
Mavere Tukai ameeleza kuwa MSD ni miongoni mwa taasisi za kimkakati na imeanza
kujiendesha kibiashara.
Tukai ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka
mmoja, MSD imeweza kuongeza hali ya
upatikanaji wa bidhaa za afya kwa kuingia mikataba ya muda mrefu na wazalishaji
ambapo upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka asilimia 51 mwaka jana wa fedha,
hadi kufikia zaidi ya asilimia 80 mwaka huu. Eneo hili pia linaonekana kwenye
kutimiza mahitaji ya wateja ambapo mwaka jana ilikuwa asilimia 44, na hii
imeongezeka na kufikia asilimia 78.
Kwa upande wa mauzo, Tukai ameeleza kuwa kuna
ongezeko la mauzo ya bidhaa za afya kutoka shilingi 77 bilioni mwaka jana wa fedha,
na kufikia shilingi 123 bilioni mwaka huu wa fedha.
Mkurugenzi huyo ameahidi kwamba MSD itaendelea kuboresha kazi zake ili kuimarisha utendaji wa kazi zake











No comments:
Post a Comment