Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe, akifungua kikao kazi cha Bohari ya Dawa (MSD) na wateja wake wakubwa.kilichofanyika jijini Dodoma Disemba 10, 2023.Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WIZARA ya Afya imeitaka Bohari ya Dawa (MSD)
kuitambua Bima ya Afya kwa wote na kuzingatia
upatikanaji wa bidhaa za afya, ubora na bei zilizo katika muongozo wa matibabu
wa Serikali.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Grace Magembe ametoa maagizo hayo Disemba 10, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha MSD na wateja wake wakubwa.
Dk.Magembe alisema MSD iwahudumie wananchi kulingana na mahitaji ya taasisi zote za afya na kuangalia mifumo ya utoaji huduma inavyoweza kukidhi mahitaji ya Bima ya Afya kwa wote.
Aidha, Naibu Katibu mkuu huyo alizitaka taasisi za afya kuangalia upya mifumo ya utoaji huduma lengo likiwa kukidhi mahitaji ya Bima ya Afya kwa wote.
“Tuangalie upya mifumo yetu ya utoaji huduma
namna inavyoweza kubadilika ili kukidhi mahitaji ya Bima ya Afya kwa
wote.Tusisumbue wananchi, muwasiliane wenyewe kwa kuwa wao wanataka hudum,”alisema.
Dk.Mgembe alisema muswada wa Bima ya Afya umepitishwa na Bunge hivyo kinachotakiwa sasa ni kuufanyia kazi kwa kutunga kanuni kwakushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Wizara ya
Fedha,Ikulu na wadau wengine.
Naye Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi alisema, kikao
hicho kitajadili changamoto na kutafuta
suluhuhisho ili MSD iweze kuwahudumia wateja wakubwa kwa bidhaa
wanazozihitaji.
“Tumeshiriki kikao cha MSD ambacho kinaunganisha
wateja wake wakubwa kutoka katika hospitali kubwa lengo ni kuboresha huduma za
kuwahudumia wananchi na kupata bidhaa wanazohitaji,..
Alisema changamoto iliyopo inatokana
na utendaji ni kwamba wateja hawa wanapokosa bidhaa MSD huagiza bidhaa zao nje ya nchi ambapo ni kinyume na sheria .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai alisema,
lengo la kuwakutanisha wateja wakubwa ni kwasababu mahitaji yao ya dawa ni makubwa tofauti na
hospitali nyingine.
Alitaja wateja ambao wamekutana nao kuwa ni Hospitali ya Kibong’oto, Muhimbili, Ocean Road, Benjamini Mkapa na Hospitali ya Mirembe.
“MSD inamikakati ya kuongeza zaidi wateja wakubwa kwa kuweka utaratibu mzuri kwa ajili ya kufanya biashara nao," alisema Tukai...
Alisema wanatengeneza mkakati wa pamoja na kuanza kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi mkubwa..
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya
Afya (NHIF) Benard Konga alisema, Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan amesaini sheria ya Bima ya Afya kwa wote na utekelezaji wake
unaanza hivi karibuni.
“Leo tumeshiriki katika kikao kilichoandaliwa na
MSD ambapo kinalengo la kutafuta suruhu ya pamoja kuhusu suala zima la upatikanaji wa dawa
nchini.
Aliongeza kuwa ili kutimiza adhma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Bima ya Afya kwa wote lazima wakae pamoja na kuwa na mikakati ambayo itafanya adhma hiyo itimie pasipo vikwazo vyovyote,
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke Dk. Joseph Kimaro alisema kumekuwa na maendeleo makubwa kwa MSD hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
“Lengo la kikao hiki ni kuimarisha ushirikiano
katika utoaji huduma za afya ambapo inaenda sambamba na uwepo wa dawa na vifaa
tiba jukumu ambalo imepewa MSD.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere , akichangia jambo kwenye kikao hicho.







No comments:
Post a Comment