Meneja wa Mradi wa armer visibility, Bw Cleophas Ntakije, akizungumza wakati akifundisha mbinu bora za kilimo cha alizeti wakati wa mafunzo kwa wadau wa kilimo.
.............................................
Na Mwandishi Wetu, Singida
MRADI wa Farmer visibility ni mradi wenye lengo la kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kidigitali kutoka katika kilimo cha mazoea na kwenda katika kilimo cha biashara na utawawezesha wakulima 100,000 katika zao la kimkakati la Alizeti katika mikoa ya Dodoma, Singida, na Manyara.
Mradi huu unafadhiliwa na shirika la Heifer International na kutekelezwa na kampuni ya Digital Mobile Africa (DMA) wenye lengo la kumuinua mkulima kidijitali kwa kulima kilimo cha kisasa, kumuunganisha na wadau wa fedha, kuwaunganisha na masoko, pia kuwapa mafunzo na taarifa mbalimbali za kilimo na hali ya hewa.
Meneja Mradi Bw Cleophas Ntakije amesema “mradi huu unalenga kwenda kutatua matatizo ya wakulima katika maeneo manne, tumegundua wakulima wadogo wadogo hawana mbinu bora za kulima alizeti, wakulima hawajaunganishwa na wadau wa kilimo ikiwemo taasisi za fedha, pia wanachangamoto ya masoko”
“Tunashirikiana kwa karibu na serikali kuanzia ngazi za kata kupitia maafisa ugani, Pia tunasapoti sera za za kilimo za serikali kupitia mazao ya kimkakati kama alizeti, hivyo nasisi tunmashiriki kwa pamoja katika ajenda ya BBTI(Jenga kesho yako iliyobora) kupitia zao la Alizeti”
“serikali pekee haiwezi kumaliza tatizo la uhaba wa mafuta hivyo tunaenda kusaidia kupunguza uhaba wa mafuta ya alizeti katika nchi yetu, mpaka sasa mahitaji ya mafuta ya kula ni zaidi ya tani 600,000 wakati uwezo wetu ni tani laki tatu (300,000)”
“Mwisho wa mradi tunategemea
mkulima atakuwa amepata uelewa mkubwa wa uzalishaji alizeti kwa tija, pamoja na
kuhakikisha wanawake na vijana wanashiriki katika kilimo bora cha Alizeti”
Fork Person wa zao mkakati la alizeti Bw Boniface Kasilalei kutoka DMA “amewasisitiza wakulima shujaa kwamba wameaminiwa basi waweze kutekeleza mradi huu na kufikisha elimu sahihi ya mradi katika vijiji vyao ili waweze kujiunga katika vikundi, ili maafisa ugani na wataalamu waweze kuwafikia kwa urahisi”.
Mratibu wa mradi wa farmer visibility mkoa wa singida Bw Abisai Simoni Malela amesema “Leo wamekutana na wakulima shujaa kutoka wilaya ya ikungi kwa ajili ya uanzishwaji wa mashamba darasa kwa zao la alizeti,kwa kutumia mbegu zilizobebeshwa ili kuwa mfano katika vijiji vyao na kuhamasisha wakulima wengine.”
Shujaa wa kilimo
kidijitali Bw Juma Shabani amesema”
wameupokea mradi kwa furaha kwasababu utaenda kuwasaidia kupata mbinu bora za
kilimo, tutaunganishwa na watoa huduma za kilimo ikiwemo wauzaji wa pembejeo na
kuletea hadi vijijini kwetu, lakini kikubwa tutaunganishwa na masoko.”












No comments:
Post a Comment