Na Dotto Mwaibale, Singida
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kintinku,iliyopo
wilayani Manyoni mkoani Singida Mateso Bwire ametoa ufafanuzi kufuatia madai
yaliyo elekezwa kwake na Mzee Salumu Mrisho akidai anawazuia watoto wake wanne ambao
ni wanafunzi wa shule hiyo kwenda kuswali siku ya Ijumaa hivyo kukosa fursa na
haki ya kuabudu.
Akitoa ufafanuzi kwa viongozi wa Baraza Kuu
la Waislam Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida ambao walifika shuleni hapo
kupata ukweli wa jambo hilo Bwire alikanusha kutowazuia wanafunzi hao kwenda
kuswali siku ya ijumaa.
“Shule yetu ipo shwari hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anazuiliwa kwenda kuswali kwani tunafuata miongozo, kanuni na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kintinku,iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida Mateso Bwire amewazuia watoto wake wannne ambao ni wanafunzi wa shule hiyo kwenda kuswali siku ya Ijumaa hivyo kukosa fursa na haki ya kuabudu.unaoelekeza namna ya wanafunzi wa dini ya kikristo na waislam wanavyo paswa kushiriki ibada wanapo kuwa shuleni,” alisema Bwire
---ANGALIA VIDEO CHINI---
0 Comments