Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (kushoto) akizungumza na Mfanyabiashara anayemiliki duka la Nagji ambaye ni msambaji mkubwa wa sukari mkoani Singida.
...........................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema kwamba wafanyabiashara
watakaobainika kuuza sukari bei kubwa kinyume na bei elekezi iliyotolewa na
serikali watafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.
Serukamba ameyasema hayo leo ( Februari 22, 2024) wakati akizungumza na
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), maafisa biashara, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote wa halmashauri za Mkoa
wa Singida baada ya kufanya operesheni ya kukagua baadhi ya maduka jumla ili kuwabaini wafanyabishara wasio waaminifu
ambao wanauza sukari kwa bei ya juu.
Alisema walichokibaini katika operesheni hiyo ni wafanyabiashara wa maduka
ya jumla wamekuwa wakiuza sukari hiyo kwa kwa kufuata bei elekezi ya Sh.14O,000
hadi 145,000 kwa mfuko wa kilo 50 lakini wanunuzi wa reja reja ndio wamekuwa
wakiiuza kwa bei kubwa.
"Niwaombe wakuu wa wilaya mkisaidiana na jeshi la polisi muende kwenye
maduka yote yanayouza sukari mkaombe bei ya manunuzi ili tujue kama walinunua
kwa bei ya kawaida au laa na waoneshe lisiti na ambaye atasema hana tumpeleke
mahakamani tumfungulie kesi ya uhujum uchumi kwa sababu risiti anayo lakini
ameificha ili akauze sukari bei kubwa," alisema Serukamba.
Aidha, Serukamba amewataka wauzaji wakubwa wa sukari kuhakikisha wanatoa risiti
kwa watu wanao wauzia ikiwa ni pamoja na kujua walipo na yalipo maduka yao
sambamba na namba zao za simu.
Katika hatua nyingine Serukamba amemuagiza Afisa Biashara Mkoa wa Singida kusimamia uuzaji wa sukari kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataanza kuipokea hivi karibuni na kuwa kinachoonekaka ni wao kuwauzia wafanyabishara wenzao ili nao waende kulangua na itakuwa vizuri sukari hiyo iuzwe kila wilaya hivyo kusaidia kuwajua wanunuzi na kuweza kufuatilia iwapo itatokea kuuzwa kwa bei ya juu.Afisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Simkwenda, akiongoza zoezi la ukaguzi wa maduka hayo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Stella Mutahibirwa.
...................................
Meneja wa TRA Mkoa wa Singida, Azaria Kasomi.
.........................
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Singida, Azaria Kasomi alisema wamejipanga vizuri kukagua risiti za mauzo ya sukari hasa kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wametembelewa leo na akatoa wito kwa wafanyabiashara hao kila wanapouza sukari watoe lisiti na atakayebainika kushindwa kuitoa atakumbana na adhabu ya kulipishwa faini ya Sh.Milioni 1.5.Ukaguzi katika duka la Vunjabei ukifanyika.
Philip Masawe ambaye pia ni mfanyabiashara aliiomba Serikali kufuatilia ukosefu wa sukari kwani haipatikani kabisa na kuwa hata ikipatikana inakuwa ni kidogo hivyo kulazimika kugawana kidogo kidogo na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni mtu mmoja tu anayeileta na wao kwenda kuinunua kwake.
Katika operesheni hiyo maduka yaliyotembelewa na kukaguliwa ni duka la Nagji, Vunja Bei, duka la Mfanyabiashara Mohsin Damji, Shemsiya, Best na dula la Mary Philipo Masawe.Ukaguzi ukifanyika duka la Shamsiya.
---ANGALIA VIDEO CHINI---
0 Comments