" />

HABARI ZA HIVI PUNDE

SOMALIA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA



Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud akisaini kitabu mara baada ya kuwasili nchini na kutembelea Bohari ya Dawa (MSD) akiwa katika ziara ya kikazi. 

....................

Na Mwandishi,  Wetu, 

RAIS wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa bidhaa za afya na kubadilishana uzoefu wa namna mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya unavyofanya kazi.

Rais Mahamud ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, ameyasema hayo alipoitembelea MSD, na kuongeza kuwa kutokana na uzoefu wa MSD, wana uhakika kuwa ubora wa bidhaa za afya utakuwa wa uhakika.

Naye Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ameeleza kuwa kwa kuwa sasa Somalia ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania kupitia MSD itaweza kununua bidhaa za afya kwa pamoja ili kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu.

Ameongeza kuwa, Marais wa nchi hizo mbili, yaani Tanzania na Somalia wamewapa maelekezo Mawaziri wa Afya nchi zao kukaa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana katika masuala ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwa urahisi, kuzingatia ubora na kwa bei nafuu.

Kiongozi huyo wa Somalia na ujumbe wake alizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya, Menejimenti ya MSD na kutembelea ghala la kuhifadhia dawa la makao makuu MSD.

Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud akiwa katika ziara hiyo ya kutembelea Bohari ya Dawa (MSD). Kulia ni Waxiri wa Afya Ummy Mwalimu.
Ziara MSD ikifanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai (kushoto) akitoa maelezo wakati wa ziara hiyo.
Utembeleaji wa ghala la kuhifadhia dawa na vifaa tiba ukifanyika.
Utembeleaji wa ghala la kuhifadhia dawa na vifaa tiba ukiendelea.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na ujumbe uliongozana na Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud.
 

No comments