Afisa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Innocent Mushi akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara mbalimbali wa jiji la Tanga kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
...........................
Na Mashaka Kibaya, Tanga
MAMLAKA ya Mapato, Tanzania (TRA) mkoani Tanga, imewataka watanzania kutambua kuwa wanapaswa kuwa Wazalendo
kwa kuhakikisha wanalipa kodi ili kusaidia katika kuharakisha maendeleo ya nchi.
Flavian Byabato, ambaye ni Afisa Mkuu Msimamizi
wa Kodi, Kitengo cha elimu na mawasiliano kwa mlipa kodi alitoa rai hiyo Machi 26, 2024 alipokuwa akizungumza kwenye kikao na Wafanyabiashara mbalimbali
Jijini Tanga.
Katika kikao hicho, Byabato alisema, kulipa kodi
ni suala la uzalendo hivyo kila mtu akiweza kutimiza wajibu wake kwa kulipa
nchi itaweza kusonga mbele katika maendeleo ikipiga hatua moja mbele kutoka
nyingine.
Byabato alitumia fursa hiyo kuhimiza matumizi
sahihi ya mashine za EFD akiwasihi wadau waliohudhuria kikao hicho hususani
Wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti halali zenye thamani halisi ya
bidhaa pindi wanapofanya mauzo au manunuzi.
Kwa mujibu wa Byabato, tayari vikao vya aina hiyo
vimeshafanyika kwa baadhi ya wilaya lengo likiwa kuzifikia wilaya zote za Mkoa
wa Tanga katika kuwapatia elimu stahiki wadau wa TRA.
Amezitaja wilaya zilizofikiwa kuwa ni Lushoto,
Handeni, Pangani, Korogwe na Muheza na
kusisitiza akisema wilaya zote za Mkoa wa Tanga zitaweza kufikiwa ili
Wafanyabiashara kuweza kuelimishwa kwa ufasaha.
Kuhusu hoja kutoka kwa wadau zilizoweza kuchomoza
mara kwa mara kwenye mikutano iliyofanyika, Byabato alisema,ni pamoja na wadau
kulalamikia suala la makadirio baadhi yao wakidai kuwa makubwa.
Hata hivyo Byabato alisema kwamba, TRA imekuwa ikifanya makadirio kwa kufuata misingi ya sheria huku
akiwasisitiza wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu zao.
Hoja nyingine aliitaja kuwa ni baadhi ya wafanyabiashara kukosa elimu sahihi ya kutumia mashine za EFD na kwamba TRA itaendelelea kutoa elimu kwa wadau wake hao ili kuweza kukuaanya
kodi.
Mjasiriamali Rose Mbelwa aliyeshiriki mkutano huo alisema, mikutano inayoendelea kuendeshwa na TRA ina umuhimu mkubwa kwa wadau kwa kuwa wanapata fursa ya kuwasilisha kero zao na kupatiwa majibu kwa
haraka.
Naye Abasi Mzee aliishauri TRA kuendelea kuwapatia elimu wadau wake hatua aliyoieleza kuwa itasaidia wananchi na nchi kuharakisha maendeleo.Viongozi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho na wafanyabiashara.Kikao hicho kikiendelea.Taswira ya kikao hicho.
0 Comments