.......................
Mashaka Kibaya, Tanga
CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kimeanzisha kituo maalum cha kulea mawazo ya
ubunifu kwa Wanafunzi lengo likiwa kuwaondosha kwenye dhana ya kuajiriwa huku
wakifikiria kujiajiri sanjari na kuweza kusaidia sehemu nyingine ya jamii.
Taarifa hiyo imetolewa Jana na Afisa uhusiano wa Chuo hicho cha uhasibu
Arusha, Stela Kalinga wakati ambapo IAA wakiwa miongoni mwa washiriki kwenye
maadhimisho ya Kimataifa ya elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024 yanayofanyika
Jijini Tanga.
Katika taarifa yake kwa Wanahabari Kalinga alisema, IAA ni mali ya Serikali
chini ya Wizara ya fedha huku kikitoa mafunzo kuanzi ngazi ya cheti,
astashahada, shahada na shahada ya uzamili.
Pamoja na hayo chuo hicho kimekuja program ya kiotamizi (incubator) kozi ya
kipekee ya elimu ujuzi inayompa mwanafunzi maarifa, ujuzi hadi kufikia nafasi
ya kujiajiri na vilevile kutengeneza mazingira ya kusaidia wengine.
Utaratibu huo umeonekana kuwa wenye
mafanikio makubwa kwa vile umeanza kutoa matokeo chanya katika kukidhi
changamoto ya ajira kwa wanafunzi kwa vile tayari wapo waliojiajiri na pia
kuweza kuajiri wenzao.
Akizungumzia zaidi program hiyo ya kipekee, Kalinga alisema,ni mtaala wa
kielimu ambapo mwanafunzi anapofika chuoni anatakiwa kuja na mawazo yake ya
ubunifu ambapo chuo kinachukua jukumu la kumuendeleza pamoja na kumuunganisha
na wadau wengine ili kumuongezea uwezo katika yale aliyoyaona kuwa ni fursa kwa
upande wake.
"Tumeanzisha program atamizi (incubator) inayolea mawazo ya kibunifu
kwa vijana na kusaidiwa kuwa vitu halisi kama biashara,sanaa, na vinginevingi,
mpaka sasa wapo waliofanikiwa kuanzisha kampuni zao" alisema Kalinga.
Kalinga aliendelea kusema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo kuanzia ngazi ya
cheti, astashahada, shahada na shahada ya uzamili mafunzo ambayo yanatolewa kwa
fani mbalimbali.
Kuhusu shahada ya uzamili,Kalinga alisema,IAA ni tofauti na vyuo vingine
kwani masomo hayo hutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja mwanafunzi anaweza
kusoma akiwa chuoni au kwa njia ya mtandao 'online'.
Kwa mujibu wa Kalinga fani zilizopo chuoni ni pamoja na uhasibu,fedha,
tehama,uchumi,kodi,utalii,masoko,bima na mengineyo na pia mafunzo ya muda mfupi
yakitolewa kwa fani mbalimbali.
Afisa uhusiano huyo ametanabaisha kuwa tayari dirisha la udahili
limefunguliwa akiwataka wakazi wa
mkoanwa Tanga na watanzania kwa ujumla kufanya maombi kupitia tovuti ya www.iaa.ac.tz kwa kuwasiliana na uongozi wa
chuo kwa simu ili kupatiwa usaidizi kufanya maombi.
Mohamedi Ramadhani Kosta ni mwanafunzi wa IAA, anasema kwamba,kupitia
utaratibu huo wa kiotamizi amefanikiwa kuanzisha kampuni yake ya kuchakata
mazao ya chakula ambapo alianza kwa kutengeneza unga wa lishe lakini kwa sasa
anauza uji wa take away huku akijivunia kuajiri vijana wenzake.
Maadhimisho ya Kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu 2024 yanafanyika katika
viwanja vya Popatlal Jijini Tanga na kauli mbiu yake ni "elimu, ujuzi na
ubunifu kwa uchumi shindani".









No comments:
Post a Comment