TAMUFO WAANDAA KONGAMANO LA KUHAMASISHA MAENDELEO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 30 May 2024

TAMUFO WAANDAA KONGAMANO LA KUHAMASISHA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel

 Mlezi wa TAMUFO, Dkt. Frank Richard

.......................

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umeandaa kongamano la siku moja linalotarajiwa kufanyika Juni 8, 2024 lenye lengo la kuhamasisha maendeleo mbalimbali.

Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel akizungumza na waandishi wa habari wameona ni vizuri kuandaa kongamano hilo kwa ajili ya kuwakutanisha wanamuzi kwa ajili ya kujadili maendeleo yao pamoja na kukumbusha baadhi ya mambo.

“Tumemwalika Apostle Bishop Dastan Maboya kama Mnenaji Mkuu ambaye atatupa neno la Mungu la la kutujenga kuhusu maadili na kuwatia moyo waimbaji ambao mbao waamejeluhiwa kwa namna moja au nyingine.

Alisema katika hatua nyingine watatumia kongamano hilo kufanya maombi maalumu ya kuliombea taifa na kuombeana wao kwa kwao.

Kwa upande wake Mlezi wa TAMUFO, Dkt. Frank Richard alisema katika kongamano hilo watakuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi zisizo za Kiserikali ambao watatoa mada na kuwa litafanyikia Ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ilala jijini Dar es Salaam.

Dkt. Richard alitumia nafasi hiyo kuwaomba wapenzi wa Muziki wa Injili na wadau wa maendeleo kujitokeza siku ambayo itakuwa na fursa za kimaendeleo zitakazo tolewa na wataalamu waliowaalika na kuwa hakutakuwa na kiingilio chochote. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad