MBUNGE AYSHAROSE AWAPA FARAJA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI SOLYA SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, May 26, 2024

MBUNGE AYSHAROSE AWAPA FARAJA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI SOLYA SINGIDA

Wanafunzi wa Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Singida ya Solya iliyopo Wilaya ya Manyoni wakionesha jezi walizokabishiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (katikati) wakati wa ziara yake ya kutembelea shuleni hapo aliyoifanya hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo Zainabu Mtinda.

 ....................................

Na Mwandishi Wetu, Singida

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida (CCM) Aysharose Mattembe amewatembelea Wanafunzi wa Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Singida ya Solya iliyopo Wilaya ya Manyoni na kuwapa faraja  na hamasa ya masomo.

Akiwahutubia wanafunzi hao wakati wa ziara yake ya kukagua shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi hao Mattembe aliwasisitiza kusoma kwa bidii na kuzingatia lengo lililowapeleka shuleni hapo na hatimaye kutimiza ndoto zao.

“ Ninyi ndio ndio waasisi wa shule hii hivyo mnatakiwa kuwa mfano bora kwa kufaulu vizuri ili kuwapa hamasa wadogo zenu ambao watajaliwa kujiunga na shule hii hapo baadaye,’’ alisema Mattembe.

Mattembe aliwaambia wanafunzi hao kwa jinsi anavyo waona anaamini wote watafaulu ufaulu wa daraja kwa kwanza na akarudia kuwasisitiza kusoma kwa bidii wa bidii ili baadaye waje kuwa kuwa viongozi wakubwa alivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani inawezekana endapo kama wataweka juhudi kubwa katika masomo yao na kuzingatia maadili.

Mhe. Mattembe alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kwajengea shule nzuri watoto wa Singida kwani shule hiyo maalum ni miongoni mwa shule kumi za vipaji zilizojengwa nchi nzima na Mkoa wa Singida ikinufaika kwa kuwa na shule hiyo.

Aidha, Mhe. Mattembe aliwapa zawadi wanafunzi hao zikiwemo taulo za kike na vifaa vya michezo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo, Zainab Mtinda awali akisoma risala yake alisema kwa kuwa shule hiyo ni mpya na ipo mbali na maduka ya Stationary wanachangamoto ya ukosefu wa photocopy, computer tatu na maabara za Biolojia, Fizikia na Kemia hazina vifaa vya kutosha vya kujifunzia ambapo  alimshukuru Mbunge Mattembe kwa kuwajali wanafunzi kwa kuwapa taulo za kike na vifaa vya michezo..

Aidha, Matembe akiwa katika muendelezo wa ziara yake hiyo Kata ya Saranda alipokea changamoto kadhaa zilizowasilishwa katika mkutano wa hadhara na diwani wa Kata hiyo, Joseph Ndahani.

Baadhi ya changamoto hizo ni ukosefu wa maji hasa katika Kitongoji cha Mbongo, Sekeula na Mankemboo, u kosefu wa Kivuko kutoka Ilalo kwenda Mankemboo, mawasiliano ya mtandao wa simu katika baadhi ya maeneo kutokuwa mazuri, uhitaji wa mabweni katika Shule ya Sekondari Saramba kwa kuwa watoto wanatembea umbali mrefu kufika shuleni, uhaba wa nyumba za walimu.

Wakisoma risala yao mbele ya Mbunge Mattembe Kikundi cha Wanawake wa Saranda (UWS) walitoa changamoto kadhaa kwa mbunge huyo ambapo waliomba kuongezewamtaji, mafunzo pamoja na viti na meza kwa ajili ya kufanyia shughuli zao wanapokutana.

Mbunge Mattembe akijibu risala hiyo aliahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo la Manyoni Mashariki Dkt. Pius Chaya.

Katika ziara hiyo Mbunge Mattembe aliambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  Wilaya ya Manyoni, Mariamu Msigwa, Katibu wa UWT Manyoni, Helena Kanijo, Madiwani wa Viti maalum ambao ni Mariamu Palingo, Blandina Mawala, Joyce Kalikawe, Neema Salum, Elizabeth Chanzi, Magreth Matonya, Amina Msita, Rehema Chizumi, na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Manyoni, Ostatila Mwilafi.

Wanafunzi hao wakionesha furaha baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo.

Mbunge Mattembe akikabidhi jezi.
Mbunge Mattembe akiwakabizi taulo za kike wanafunzi hao.
Wanafunzi hao wakipiga makofi kufurahia msaada huo kutoka kwa Mbunge Mattembe.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad