MBUNGE AYSHAROSE AGAWA VYANDARUA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, May 26, 2024

MBUNGE AYSHAROSE AGAWA VYANDARUA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI

Mbunge  wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe (katikati) akigawa vyandarua Hospitali ya Wilaya ya Manyoni wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni.

..............................

Na Mwandishi Wetu, Singida

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Manyoni na kukagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto.

Akizungumza lengo la ziara hiyo Mattembe alisema ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alitembea na kukagua ujenzi wa jengo hilo na kutoridhishwa na kasi ndogo ya ujenzi.

"Niwaombe kuongeza kasi ya jengo hili la Mama na Mtoto ili liweze kumalizika haraka na kuanza kutoa huduma ya mama na mtoto na kuhimarisha afya zao," alisema Mattembe.

Aidha, Mattembe katika ziara hiyo Hospitali hapo aliweza kugawa vyandarua ambapo aliwataka waliobahatika kugaiwa wakavitumie kwa ajili ya kuwasaidia kuzuia maambukizi ya malaria na si kwamatumizi mengine.

Mbunge Mattembe akimgawia chandarua mmoja wa wagonjwa aliyekuwa akipatiwa matibabbu kwenye Hospitali hiyo.
Mashuka na vyandarua vikikabidhiwa na Mbunge Mattembe.
Mbunge Mattembe akiwa amembeba mtoto wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea hospitali hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad