MILIONI 987.7 KUMALIZA KERO YA MAJI NG'ANG'ANGE, MDEKE, WANANCHI WAMSHUKURU MBUNGE WAO NYAMOGA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 18, 2024

MILIONI 987.7 KUMALIZA KERO YA MAJI NG'ANG'ANGE, MDEKE, WANANCHI WAMSHUKURU MBUNGE WAO NYAMOGA


Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya ujenzi wa mradi wa maji katika Vijiji vya Ng'ang'ange na Mdeke wilayani Kilolo mkoani Iringa.

...........................

Na Mwandishi Wetu, Iringa

Hatimaye kilio cha kero ya maji kiliochokuwa kimewagubika wananchi wa vijiji vya Ng’ang’ange na Mdeke Jimboni Kilolo kitamalizika baada ya Serikali kutoa Sh987.7 milioni na kutia saini ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo.

Tayari  Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mkoani Iringa na Mkandarasi  Africantric  Co. Ltd  wametia saini ya mkataba kwa ajili ya kuanza mradi huo.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini wa mradi huo amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha  wananchi wake wanapata maji safi na salama.

Mbunge wa Kilolo, Mh Justine Nyamoga ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo kubwa. “Leo mkataba wa ujenzi wa mradi huu umesainiwa, namshukuru sana Rais Dk Samia Suluhu Hassan, naishukuru Serikali kutukumbuka wana Ng’ang’ange na Mdeke,”

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Maji wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Maji, Mh Anna Lupembe wameshuhudia utiaji huo wa saini.

Viongozi wengine ni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kilolo wakiongozwa na  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve, Madiwani wa Wilaya ya Kilolo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Anna Msola pamoja na viongozi wa RUWASA.

Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa Saini ya ujenzi wa mradi wa maji Ng'ang'ange na Mdeke.Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kudo Mathew akizungumza baada ya utiaji wa saini ya ujenzi wa mradi wa maji katika vijiji vya ng'ang'ange na Mdeke Wilayani Kilolo mkoani Iringa. Wananchi wa Kijiji cha Ng'ang'ange wakiwa kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad