Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amesema hayo
alipokuwa akifungua rasmi kikao kazi cha
cha wadau na wateja wa MSD mkoa wa Katavi wanaohudumiwa na MSD Kanda ya
Tabora.
Aidha ameipongeza menejimenti ya MSD kwa kuendelea kuboresha upatikanaji wa
bidhaa za afya nchini, kwani kiwango kimekuwa kikiongezeka siku hadi siku.
Kwa upande mwingine amewaagiza waganga Wakuu wa Wilaya na Wafamasia
kufuatilia matumizi sahihi ya bidhaa za afya kwenye kila ngazi ili kuhakikisha
usimamizi mzuri unazingatiwa.
Naye Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji kutoka MSD Victor Sungusia, ameeleza
maboresho mbalimbali yaliyofanywa na MSD kiutendaji, ikiwa ni pamoja na
ongezeko la kukidhi mahitaji ya wateja kutoka asilimia 40 mwaka 2021/2022 hadi
kufikia asilimia 86 sasa.
Aidha amebainisha juhudi mbalimbali za MSD katika kuongeza maeneo ya
Uhifadhi katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na jitihada za uzalishaji wa
bidhaa za afya nchini.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Waganga
wakuu wa Halmashauri, wafamasia, wataalam wa maabara, Waganga Wafawidhi na Mameneja wa Hospitali za
wilaya za mkoa wa Katavi.


















No comments:
Post a Comment