MKUSANYA USHURU MANISPAA YA SINGIDA ATIWA HATIANI KWA KUJIPATIA MANUFAA YA TSH. 2,043,800/= - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 18, 2024

MKUSANYA USHURU MANISPAA YA SINGIDA ATIWA HATIANI KWA KUJIPATIA MANUFAA YA TSH. 2,043,800/=


.................................

 Na Mwandishi Wetu, Singida. 

MAHAKAMA ya Wilaya ya Singida imemhukumu aliyekuwa Mkusanya Mapato kwa kutumia mashine ya POS ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Bw. Kitwana Hamisi Tamba

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la Matumizi mabaya ya madaraka ambalo ni kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Kitwana Hamis Tamba katika shauri la Uhujumu Uchumi Na. 07/2023, imetolewa na Mhe. Fadhil Luvinga - Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida - Mei 16, 2024.

Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya Shilingi 100,000/=, kufidia Jamhuri Shilingi 500,000/= na kurejesha Tsh 2,043,800/= katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Mshtakiwa huyo alijipatia manufaa ya Shilingi 2,043,800/=  kupitia makusanyo ya fedha kwa njia ya POS ambapo alikuwa akikusanya ushuru katika stendi kuu ya Mabasi Misuna iliyopo Manispaa ya Singida.

Mshtakiwa amelipa faini na fidia. Pia amerejesha fedha katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad