MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI MBEZI LAWAMANI KWA UBABE, ACHANGISHA FEDHA ZA MTIHANI BILA VIKAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 28 May 2024

MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI MBEZI LAWAMANI KWA UBABE, ACHANGISHA FEDHA ZA MTIHANI BILA VIKAO

Muonekano wa baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Mbezi jijini Dar es Salaam.

 .................................

Na  Waandishi Wetu, Dar es Salaam 

Baadhi ya wazazi na wadau wa elimu katika Manispaa ya Ubungo, kata ya Mbezi Mwisho wamemtuhumu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi na Ufundi, Manispaa ya Ubungo , kata ya Mbezi kwa ujeuri, kiburi na kugombana na wazazi wa eneo hilo kuhusu matatizo mbalimbali ya shuleni hapo ikiwamo fedha za masomo ya ziada (Tuition), gazeti linaripoti.

 Akizungumza na waandishi wetu jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo hakutaka jina lake litajwe mmoja ya wazazi alisema kwamba (Jina Kapuni) alisema kwamba Mwalimu Mkuu huyo Daniel Machage ni mjeuri, kiburi na hana ushirikiano na wazazi kuhusu matatizo mbalimbali shuleni hapo.

“Kuna kipindi Fulani huko nyuma kwenye kikao cha uongozi wa shule na wazazi alitaka kupigana hadi kuguchana na mmoja ya wazazi baada ya mzazi kuhoji pesa ya masomo ya ziada (Tuition),”

“Mmoja ya wazazi aliuliza je kama sina fedha za masomo ya ziada mwanangu hawezi kuingia darasani alijibu kwa kiburi na dharau ndio wakataka kupigana mpaka walimu na wazazi wengine wakaingilia kati,’ alisema Mzazi kwa masikitiko makubwa

Aliongeza kwamba Mwalimu Mkuu huyo hana nidhamu na hataki kushirikiana na wazazi kwa sababu shuleni hapo kuna tatizo kubwa la maji na watoto wanasoma bila maji hapo na wakienda kujisaidia hakuna maji kabisa.

Alisema kwamba awali maji yaliwepo shuleni hapo ila Mwalimu huyo mkuu aliacha kulipa bili za maji akisema kwamba ni kubwa sana na wanafunzi ni wengi hawezi kuendelea kuingia gharama hizo hata alivyoelezwa kwamba wazazi wapo tayari kuchangia maji alikataa.

Mzazi huyo aliendelea kusisitiza kwamba pamoja na kiburi na jeuri lakini hataki kusikiliza maoni ya wazazi ambapo watoto wao wanasoma shuleni hapo,

“Miaka kama mitatu nyuma kuna mtoto aliwahi kufanyiwa vitendo vibaya na baadhi ya wapiti njia kwa sababu shuleni hapo hakuna ukuta ambapo unaweza kuwatenganisha wanafunzi na watu wa mitaani,’ alisisitiza

 Kwa upande wake mdau mwingine wa elimu ambaye hakutaka kutajwa alisema kwamba kuna tuhuma za mwalimu mkuu huyo kwamba anafanyavunyanyasaji kwa walimu hasa wa kike.

Mtoa taarifa mwingine alidai kwamba kuna taarifa zinadai kwamba amekuwa na tabia ya kukusanya michango kutoka kwa wanafunzi bila kuwa na kikao na wazazi kama vile mwongozo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tamisemi unavyotaka.

Taarifa za awali zilidai kwamba Mwalimu Mkuu huyo ni mbabe ana kiburi , anatoa lugha zisizo na staha kwa walimu wa kike na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili kwa viongozi wa umma.

Alipotafutwa na waandishi wa habari hizi , Mkuu huyo wa shule , Bw Machage alisema kwamba kwamba michango yote kwa ajili ya mitihani ya mihura na moko inafanywa baada ya kikao cha wazazi kuridhia kama muongozo wa wizara ya elimu na  Mafunzo ya  Ufundi unavyotaka.

Bw Machage  aliongeza kwamba kila mwezi wa Juni huwa wanafanya kikao na wazazi shuleni hapo ili kuweza kujadiliana kwa kina kuhusu matatizo na changamoto za shule na kuweza kutafuta majawabu kwa pamoja.

“sio kweli mimi nakusanya michanho kwa wanafunzi kupitia wazazi wao bila kufanya nao vikao huwa tunakuwa na vikao hapa tena safari hii nitawaalika kwenye kikao cha mwezi wa sita huwa nafunga (Speakers) mpaka kule stendi ya magufuli wanasikia,” alisema.

Aliongeza kwamba ni kweli fedha kutoka serikalini  zinakuja kupitiaTamisemi kiasi cha shilingi 1.2 milioni kila mwezi ila ni kwa ajili ya ukarabati wa shule ,miundombinu , vifaa na mambo ya michezo.

Alifafanua kwamba  pamoja na mambo mengine lakini fedha hizi hazitishi na kwa kweli siwezi kukusanya fedha bila idhini ya wazazi, ,Mkurugenzi na kibali cha Mkuu wa Wilaya (DC).

“Katika  hiyo fedha 1.2 millioni utoe 2% ili uweze kugharamia mitihani ya mihura, moko na ya kata kwa wanafunzi wasipoungua 2,532 na darasa la saba pekee ni wanafunzi 291 hii (capitation) yaserikali haiwezi kutosha ndugu zangu,”alisisitiza kwa sauti yaupole

Aliendelea kusema kwamba Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  yaUbungo ingawa hakutoa maandishi ila yatakuja alisema kwamba kwa madarasa ya mitihani kila wiki wanaweza kuchangia 1500 na kwa madarasa ambayo hayana mitihani kila mwezi 1000.

“Sasa sie hapa tunajibana kwa fedha ya madarasa ambao hawana mitihani ya kila wiki na tunakusanya kila mwezi na  kugharamia mitihani ya kata kwa sababu hatukusanyi michango kwa ajili ya mitihani ya kata kutoka kwa wazazi,” alisema kwa kujiamini

Akifafanua juu ya tuhuma hizo alisema kwamba sio kweli kwamba yeye ana tumia lugha mbaya ni kusimamia kanuni, sheria na taratibu za serikali katika kuhakikisha taaluma inapanda shuleni hapo,

 “Kama mimi ningekuwa na mahusiano mabaya na walimu wangu nisingeweza kupandisha kiwango cha ufaulu wa shule hii kwa sababu ufaulu unapanda shule hii ni ya 20 kati 80 katika Wilaya ya Ubungo tunakwenda vizuri kwa kweli,” aliongeza

 Kwa Upande wake, Afisa Elimu wa Wilaya yaUbungo, Ndugu Denis Nyoni alinukuliwa akisema kwamba michango yote inayokusanywa shule lazima kuwe kumefanyika vikao kati ta wazazi na uongozi wa Shule na wazazi kuridhia kuchangia gharama za elimu.

 “sikia ndugu yangu fedha za serikali zinakwenda kila mwezi ila pale am ambapo hapakutosha wanaweza kukusanya michango kama waraka wa serikali unavyosema na kibali kinatoka kwa Mkuu wa Wilaya (DC) na si vinginevyi,” alisisitiza Ndugu Nyoni.

  Ndugu Nyoni  aliongeza kwamba taratibu zote za serikali zinafuatwa na sio kweli kwamba Mwalimu Mkuu huyo hapo Mbezi anafanya mambo kwa matakwa yake na mengine watu wanakuwa na maslahi yao kwa kweli ila kama kuna tofauti naweza kufuatilia.

 Kwa Upande Mratibu wa Elimu Kata ya Mbezi, Bi Suzana Massawe alisema kwamba kwa upande wake hajapata malalamiko hayo ya ukusanyaji wa michango kwa ajili mitihani shuleni hapo ila atafuatilia

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad