......................................
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bi.Mwamini Malemi, amewataka wafayakazi wa mfuko huo kuboresha huduma bora kwa wnachama wa mfuko huo.
Malemi alitoa maagizo hayo wakati akifungua Mkutano wa 52 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF. Jijini Mwanza Mei 9, 2024,
" Boresheni huduma bora kwa wanachama, wajengeeni uwezo wafanyakazi, ongezeni kasi ya ukuaji wa mfuko kwa kuifikia sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi wenu," alisema Malemi.
Aidha, Malemi alisema NSSF itaendelea kusimamia maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, na kuhakikisha Watanzania waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wanasajiliwa na mfuko na waajiri wanawasilisha michango stahiki ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Alisema lengo la mkutano huo ni kupitia mpango wa mwaka ujao na Bajeti kwa mwaka 2024/25, ikiwa ni ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi ya kiutendaji.
Mkutano huo ulifanyika Mei 9, 2024 Hoteli ya Malaika Jijini
Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Mkutano




















No comments:
Post a Comment