DC KATWALE AWATAKA WATOA HUDUMA KWENYE MABASI KUZINGATIA UBORA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 11, 2024

DC KATWALE AWATAKA WATOA HUDUMA KWENYE MABASI KUZINGATIA UBORA

Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini,  Deusdedith Katwale akizungumza na wadau wa usafirishaji mkoani humo wakati akifungua mafunzo kwa wahudumu wa mabasi.

....................................

Na Nyamizi Moses, (Singidani Blog )Tabora

MKUU wa Wilaya ya Tabora mjini,  Deusdedith Katwale amewataka watoa huduma kwenye Mabasi ya abiri kuzingitia Sheria na taratibu za usafirishaji wa abiria Ili kutoa huduma zilizo bora Kwa wasafiri.

Katwale ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya huduma bora kwa wahudum wakati akifungua mafunzo ya huduma bora kw u wa Mabasi yanayotolewa kwa siku tano wilaya hapa chini ya Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) wakishirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Katwale amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga zaidi ya Sh. Bilion 49 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya usafiri kwa watanzania Ili waweza kusafiri salama bila changamoto yoyote  hivyo ametaka mafunzo hayo yakawe chachu ya mabadiliko kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria na kuifanya huduma hiyo kuwa bora kama  huduma za usafiri wa Anga.

Aidha, Katwale amewaasa wamiliki wa vyombo vya usafiri kushirikiana na watoa huduma Ili kuifanya huduma hiyo kuwa bora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mabasi yanakuwa na ubora wa hali ya juu  na sio kuwa na mabasi mabovu ambayo yatakuwa kero kwa wasafiri,

Kwa Upande wake mkuu wa idara ya usafiri salama kutoka chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji, Patrick Makule amesema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma zinazotolewa kwenye Mabasi zifanane na huduma zinazotolewa kwenye vyombo vingine vya usafiri kama Ndege na Meli.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa LATRA Nchini, Nelson Mmari ambaye ni Afisa Mfawidhi wa LATRA mkoani Tabora amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri wa mabasi kuhakisha watoa huduma wa ndani ya Mabasi wawe wamepata mafunzo yanayotolewa na mamlaka husika na adhabu itatolewa Kwa chombo husika endapo ikagundulika mhudumu wake hana cheti cha mafunzo ya usafirishaji

Mafunzo hayo yakiendelea.
Taswira ya mafunzo hayo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad