TANZIA
Mwandishi wa Habari wa Mtandao wa Singidani Blog, Ndugu Dotto Mwaibale, anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Ndugu Hebroni Mwaibale, kilichotokea jana Mei 14, 2024 asubuhi nyumbani kwake Chang'ombe Jijini Dodoma ambapo mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na leo Mei 15, 2024 mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kijiji cha Segera Lutengano wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa mazishi yatakayo fanyika kesho Mei 16, 2024. Marehemu ameacha watoto sita na wajukuu kumi. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina lake Lihimidiwe.










No comments:
Post a Comment