Mhadhiri Dkt. James Zotto wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akizungumza wakati wa utambulisho wa kitabu kinachohusu utangamano wa Afrika na changamoto zake.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Kenya
Wahadhiri wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini
Tanzania, wametua Nairobi, Nchini Kenya
kutambulisha kitabu walichoandika kuhusu
matarajio ya utangamano kwa kutumia mgogoro wa Sahara Magharibi kama moja ya
changamoto kufikia utangamano wa bara la Afrika.
Wahadhiri hao Dk Maxmillia Chuhila na Dk James Zotto wamekitambulisha
kitabu chao ambacho kimehaririwa na
kuchapishwa na APE NETWORK katika hafla
iliyofanyika Chuo Kikuu cha Kenyatta, jijini Nairobi nchini Kenya.
Hivi karibuni Zotto na Dk Chuhila
walifanya uzinduzi wa kitabu hicho katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU), Mkoani
Iringa nchini Tanzania.
Utambulisho wa kitabu hicho nchini Kenya unalenga kusambaza maudhui ya
utangamano wa Afrika kwenye nchi za bara hilo huku kikichambua changamoto
zinazo kwamisha Muungano wa Afrika.
Akizungumza katika wasilisho lake, Zotto amesema unahitajika
ushirikiano wa pamoja wa Waafrika katika kufikia ndoto za utangamano
licha ya kuwepo kwa tofauti za kikabila,
lugha, tamaduni, Mila na desturi.
Kulingana na wanazuoni hao, umoja na utangamano ni silaha laini ya
kukabiliana na tishio lolote kutoka mataifa mengine.
Mawasilisho yao yameonesha kuwa eneo la Sahara limeona maendeleo ya kijamii
na kiuchumi kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali ya Morocco, na kuifanya
kuwa kitovu cha maendeleo na uwekezaji.
Wanahistoria hao wawili walitoa wito kuwepo kwa mazungumzo madhubuti na
yenye kujenga ili kukomesha mzozo huo wa
muda mrefu kwa kuzingatia juhudi zilizofanywa na Umoja wa Mataifa na umoja wa
Afrika kumaliza mzozo huu wa kihistoria.
Dk Chuhila ambaye ni Mwenyekiti wa
Historia Tanzania amessisitiza kwamba suluhu ya mgogoro huo inatakiwa
itoke ndani ya watu wa Morocco wenyewe na wale wa Sahara Magharibi.











No comments:
Post a Comment