WANANCHI IKUNGI WAOMBWA KUHUDHURIA KAMBI YA MATIBABU YA MAMA SAMIA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, May 11, 2024

WANANCHI IKUNGI WAOMBWA KUHUDHURIA KAMBI YA MATIBABU YA MAMA SAMIA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Thomas Apson  

.................................

Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog

MKUU wa Wilaya ya Ikungi Mkoawa  Singida, Thomas Apson akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi wanawaomba Wananchi wa wilaya hiyo  kuhudhuria kambi ya matibabu ya Mama Samia.

Apson ametoa ombi hilo jana alipokuwa  akizungmza na waandishi wa habari kuhusu matibabu yatakayotolewa wakati wa kambi hiyo ya siku nneitakayoanza kesho kutwa Jumatatu..

"Tunapenda kuwatangazia wananchi wote wa Wilaya ya Ikungi na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na Kambi ya Matibabu ya Mama Samiaitakayofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi iloyopo karibu na ofisi za mkuu wa Wilaya kuanzia Mei 13, 2024  mpaka Mei 17, 2024," alisma Apson.

DC Apson alisma huduma zitakazotolewa ni pamoja na Madaktari Bingwa wa watoto, Madaktari Bingwa wa wanawake, Madaktari Bingwa wa Upasuaji, Madaktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ikiwemo Figo, Moyo, kisukari na mengineyo, Madaktari Bingwa wa kinywa na Meno, Tohara kwa watoto na wanaume.

Alisema huduma zote zitatolewa kwa gharama nafuu ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote ili wanufaike na huduma hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad