Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Bw. Anthony
Mtaka akizungumza na Makundi ya Kianamama, vijana na makundi maalumu wakati
Baraza la Uwezeshaji Wananchi (NEEC)lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi
na Mama Samia mkoani humo kwa lengo la kutoa uwezeshaji kwa makundi hayo,
wakwanza kushoto ni katibu Mtendaji wa
baraza hilo, Bi. Beng’I Issa, wa pili kushoto Katibu Tawala Mkoa wa Njombe,
Bi.Judica Omari, wa pili kulia ni Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi.
Sophia Mjema, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya NJombe, Bi. Kissa Kasongwa. Picha
na Mwandishi wetu, Njombe.Na Mwandishi
Wetu, Njombe
BARAZA la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia Program ya
Imarisha Uchumia na Mama Samia (IMASA) imejipanga kutoa uwezeshaji kwa makundi
ya kinamama, vijana na makundi maalumu ya Mkoa wa Njombe ili waweze kuongeza
uzalishaji wa mazao yenye masoko nje ya nchi yaweze chochea upatakanaji wa
fedha za kigeni hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji,Bi. Beng’i Issa wakati alipokuwa
akizunguza na makundi ya akinamama, vijana na makundi maalumu jana Mkoani humo,
kuwa IMASA imalengo kutoa uwezeshaji kwa mazao wanayozalisha yawe chachu ya
kupata fedha za kigeni.
“Mkoa huu wa njombe ni muhimu sana sababu wananchi wanazalisha mazao
ya biashara ambayo masoko yake yapo nje ya nchi na hii inasaidia kutuingizia
fedhaza kigeni katika taifa letu,” na
aliongeza kusema IMASA imejipanga
kuwawezesha ili waweze kuongeza uzalishaji.
Alisema mazao yanayozalishwa na kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi ni
pamoja na kilimo cha miti kuzalisha mbao, kilimo cha zao la parachichi na
vilevile mazao ya viazi na mazao hayo
yanamasoko nje ya nchi.
Alisema mkoa huo ulipokea program hiyo vizuri na wengi walijitokeza
kujiunga katika kanzi data ya baraza ukilinganisha na mikoa mingine ili kupata
uwezeshaji na walioshiriki katika program hiyo ni wananchi 700.
Alifafanua kwamba mkoa huo unahalmashauri za wilaya nne na kila
halmashauri iliwakilishwa vizuri ili kupata elimu namna ya kujiunga kwa ajili
ya kupata uwezeshaji na kwenda kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara.
Alisema uwezeshaji unaohitajika ni kusaidia mazao wanayozalisha yaweze
kuongezewa thamani, mfano mazao ya mbao
takataka zake ziweze kupata mashine ya kuziendeleza ziweze kutumika kwa
matumizi ya binadamu.
Pia alisema zao la parachichi linauzwa kabla halijaongezwa thamani nje
ya nchi hivyo program itawezesha upatakanaji wa mashine kwa ajili ya
kuliongezea thamani zao hilo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Anthon Mtaka alisema programa hiyo
imekuja wakati mwafaka na mkoa wake umejipanga kutekeleza na kuhakikisha
matunda yake yanapatikana.
“Rais wetu wakati wote anazungumza biashara na uchumi hivyo na sisi
wajibu wetu kumsaidia ili taifa hili liweze kusonga mbele kiuchumi,” sekta
binafsi imepata kiongozi sahihi sababu ndiyo inayoajiri watu wengi alisisitiza.
Akitoa mfano alisema eneo linaloajili watu wengi ni kilimo, ufugaji na
uvuvi na serikali imeweka ruzuku hivyo wananchi wanahitajika kutumia fursa
mbalimbali zilizopo katika mkoa huo kukuza mitaji na kuwa matajiri.
Pia aliwataka viongozi na watumishi mbalimbali katika mkoa huo
wakatumie elimu hiyo kuwaelimisha wanachi kutumia fursa hiyo kuweza kuzalisha
mazao kibiasharana kuondokana na umasikini na siyo kubaki maofisini bali
wasaidie wananchi.
Alisema mkoa huo akinamama wanathubutu, wanauza viazi mviringo,
wanashamba miti na anzalisha mbao na wanabodaboda na kwenye vumbi la mbao
watengeneza bidhaa ni wachapakazi, kazi ni kuwaambia fursa hizo na mabenki
kuwawezesha.
Mshauri wa Rais Katika Mambo ya Kinamama, Bi.Sophia Mjema alisema
akinamama, vijana na makundi maalum wanahitajika kutumia IMASA ili kuweza
kupata uwezeshaji na kuboresha shughuli za biashara na ujasirimalia.
Na Mwaanchi ,Bi.Sala Kile toka Wilaya a Njombe alisema anaamini kuwa programa hiyo itasaidia sana katika shughuli zao za ujasirishaji ili kuendeleza familia zao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa akizungumza na Makundi ya Kianamama, vijana na makundi maalumu) wakati baraza hilo lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani Njombe kwa lengo la kutoa uwezeshaji kwa makundi hayo, watatu kutoka kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Bw. Anthony Mtaka, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Bi.Judica Omari, wa tatu kutoka kulia ni Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi. Sophia Mjema na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya NJombe, Bi. Kissa Kasongwa. Picha na Mwandishi wetu, Njombe.
Mshauri wa Rais wa Masuala ya Wanawake,Bi. Sophia Mjema katikati akiwa na makundi ya akinamama, vijana na makundi maalumu Mkoani Njombe wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi (NEEC)lilipopeleka Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani humo kwa lengo la kuwafikishia uwezeshaji makundi hayo, kulia kwake ni katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’I Issa. Picha na Mwandishi wetu, Njombe.
Mshauri wa Rais wa Masuala ya Wanawake, Bi. Sophia Mjema akiwa katika soko Kuu la Mkoa wa Njombe alipotembelea shughuli za biashara zinazofanywa na makundi ya kinamama, vijana na makundi maalumu Mkoani Njombe wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi (NEEC)lilipopeleka Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) mkoani humo kwa lengo la kuwafikishia makundi hayo uwezeshaji, nyuma yake ni katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa. Picha na Mwandishi wetu, Njombe. Picha na Mwandishi wetu, Njombe.











No comments:
Post a Comment