Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol
wameshuhudia utiaji saini Mkataba (1) Hati za Makubaliano (2) na Tamko la
Pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi (1) kwenye hafla
iliyofanyika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na
Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati
wakishuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong
wakisaini Tamko la Pamoja kuhusu Uanzishwaji wa Majadiliano juu ya Mkataba wa
Ushirikiano Kiuchumi. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo
tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na
Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati
wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
January Makamba pamoja na Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha (Jamhuri ya Korea) Choi Sang Mok
wakisaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea kuhusu Mkopo
unaotolewa na Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea
(Economic Development Cooperation Fund-EDCF). Hafla ya utiaji saini imefanyika
katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na
Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati
wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
January Makamba pamoja na Waziri
wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakibadilishana Hati ya Makubaliano kati ya
Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Biashara,
Viwanda na Nishati ya Jamhuri ya Korea kuhusu Ushirikiano katika Madini ya
Kimkakati. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02
Juni, 2024.

No comments:
Post a Comment